Utafiti mpya unaonyesha kuwa inzi wa kiume wanaokunywa pombe huvutiwa zaidi na nzi wa kike
Kwa kuongeza pombe kwenye chakula cha wadudu hawa wa kiume, hutoa kemikali nyingi zaidi ambazo huongeza mvuto wa ngono, na kuwafanya kufanikiwa zaidi katika kujamiiana.
Nzi wanaopenda matunda, wanaojulikana kwa jina la kisayansi la Drosophila melanogaster, mara nyingi hupatikana kwenye mapipa ambapo chakula kilichotupwa hukusanywa. Chakula chao ni matunda yanayooza ambayo polepole hubadilika kuwa chachu na kuwa kama pombe.
Wanasayansi wamejaribu kuchunguza kwa nini wanavutiwa na vilevi na athari zake kwao.
Utafiti uliopita ulizingatia maoni mbalimbali kuhusu mvuto wa vilevi (alcohol). Miongoni mwa dhana hizo ni kwamba lengo la nzi lilikuwa kufikia hali ya kuridhika au kupata raha ile ile ambayo inzi wa kiume hupata wakati wa kujamiiana wanapokataliwa na wanawake.
Bill Hansen, mkuu wa sayansi ya mageuzi ya neva katika Taasisi ya Max Planck, ambaye aliongoza uchunguzi huo, anasema kwamba utafiti huo unaonyesha kwamba tabia ya nzi ni sawa na ya wanadamu. Hata hivyo, pia anadai kuwa utafiti wake unaonyesha kuwa unywaji huwapa nzi faida ya uzazi.
"Hatufikirii sababu ya nzi kunywa vilevi ni kwa sababu hawana furaha," anasema.
Pia anasema kuwa kivutio cha nzi kwa wanga na chachu iliyo katika matunda yanayoharibika, pamoja na vilevi , haiwezi kutenganishwa.
Utafiti huo umebaini kuwa vilevi kwa ujumla, hasa methanol, huongeza uzalishaji na utolewaji wa kemikali za ngono ziitwazo pheromones katika inzi dume, hivyo kuwafanya wavutie zaidi wanawake.
Pheromones hutolewa angani kutoka kwa mdudu mmoja, na kuathiri tabia ya mdudu mwingine wa aina hiyo hiyo.
Kwasababu hii, wanaume huonyesha tamaa kali ya kilevi, na huonekana kwa nguvu zaidi kati ya nzi ambao hawajafanya ngono hapo awali.
Matokeo mengine ya utafiti huo mpya ni kwamba mwitikio wa nzi kwa kunusa vilevi hudhibitiwa na mizunguko mitatu tofauti ya neva katika ubongo.
Mizunguko miwili kati ya hizi ina jukumu la kuvutia inzi wa kiume kwa kiasi kidogo cha pombe, wakati wa tatu ni wajibu wa kuhakikisha kwamba wanafukuzwa na kiasi kikubwa cha pombe.
Kwasababu kilevi ni sumu, ubongo wa nzi huzingatia hatari na manufaa ya kuinywa, kusawazisha ishara za mvuto na chuki.
"Hii inaonyesha kwamba nzi wana utaratibu wa kupata faida zote za kunywa pombe bila hatari ya kulewa," anasema Ian Keese wa Chuo Kikuu cha Nebraska, mwandishi mkuu wa utafiti huo.
Katika uchunguzi wao, watafiti walichanganya masomo ya kisaikolojia, kwa kutumia mbinu za kupiga picha ili kuibua michakato ya ubongo wa nzi, na uchambuzi wa kemikali wa harufu katika mazingira na kusoma mifumo ya tabia.
0 Comments