Header Ads Widget

NYWELE BANDIA MARUFUKU 'MISS IVORY COAST'

 


Marlène-Kany Kouassi ni mmoja wa washindi wawili pekee wa taji la Miss Ivory Coast katika kipindi cha zaidi ya miongo sita waliovaa taji lao juu ya nywele zao za asili.

Nywele za bandia au mawigi yamekuwa yakitawala katika mashindano maarufu ya urembo nchini Ivory Coast kwa miaka mingi.

Hivyo, Washiriki nchini humo hutumia kiasi kikubwa cha fedha kujiandaa kuanzia mavazi hadi mitindo ya nywele huku wachache sana wakichagua muonekano wa asili.

Kwa zaidi ya miongo sita, kumekuwa na mifano miwili tu ya kipekee ya hivi karibuni ya Marlène-Kany Kouassi, aliyeshinda taji la Miss Ivory Coast mwaka 2022 akiwa amependeza kwa nywele zake fupi za asili.

Ushindi wake haukuwa wa kipekee tu nchini Ivory Coast bali hata duniani kote, ambako viwango vya urembo vya Magharibi mara nyingi hutazamwa kama ndivyo vinavyotakiwa na washiriki na hata majaji.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI