Header Ads Widget

MKUCHIKA: KIGOMA YA SASA SIYO KAMA YA ZAMANI

 

             Shule ya Sekondari ya Wasichana Kigoma iliyopo wilaya ya Uvinza mkoani Kigoma

Na Fadhili Abdallah, Kigoma

WAZIRI wa nchii ofisi ya Raisi Ikulu Kazi Maalum George Mkuchika amemaliza ziara yake ya kiserikali ya siku nne mkoani Kigoma na kubainisha kuwa mkoa11 Kigoma umepiga hatua kubwa za maendeleo na kwamba Kigoma ya sasa siyo kama ile ya zamani.

Mkuchika alisema hayo akizungumza na Jumuia ya Wanafunzi, walimu na watumishi wa Halmashauri ya wilaya ya Uvinza ambapo Waziri Mkuchika alisema kuwa ameshuhudia miradi mikubwa yenye thamani kubwa ambayo inalenga kuleta maendeleo kwa wananchi wa mkoa Kigoma.

Akiwa katika ziara hiyo mkoani Kigoma Mkuu Waziri Mkuchika alishuhudia utekelezaji mkubwa wa maji katika manispaa ya Kigoma Ujiji wenye thamani ya shilingi Bilioni 42 ambao umekamilika, mradi wa maji wa vijiji nane wilaya ya Buhigwe wenye thamani ya Shilingi Bilioni 9.7, mradi mkubwa wa maji kwa ajili ya wakazi 187,000 wa mji wa Kasulu wenye thamani ya shilingi Bilioni 35 sambamba na mradi wa maji kwa mji wa kibondo wenye thamani ya shilingi Bilioni tano.



WAZIRI wa nchi ofisi ya Rais Ikulu Kazi Maalum George Mkuchika akihutubia mkutano wa hadhara wa wananchi katika kijiji cha Busunzu wilaya ya Kibondo mkoani Kigoma akiwa kwenye ziara ya kiserikali ya siku nne mkoani Kigoma.

 Sambamba na hayo Waziri Mkuchika alitembelea na kukagua mradi wa barabara ya kiwango cha lami ya Manyovu wilaya ya Buhigwe hadi Kabingo wilaya ya Kakonko kilometa 260 ambao alisema kuwa umekuwa kichocheo kikubwa cha mabadiliko na maendeleo ya kiuchumi kwa mkoa Kigoma na wananchi wa mkoa huo. 


Alisema kuwa utekelezaji wa miradi uliofanyika miaka minne ya Raisi Samia ikiwemo ambayo amemalizia iliyoachwa na mtangulizi wake  ni kielelezo halisi cha utashi wa Raisi Samia katika kuwaletea wananchi wa mkoa Kigoma maendeleo baada ya mkoa huo kulalamika kuachwa nyuma kimaendeleo na kwamba amethibitisha kuwepo na maendeleo makubwa ya mkoa huo katika kutekeleza miradi kutekeleza mpango wa maendeleo ya kiuchumi ya mkoa.

Akizungumzia ziara ya waziri Mkuchika mkoani Kigoma, Mkuu wa mkoa Kigoma, Thobias Andengenye alisema kuwa imeamsha ari ya watumishi katika kutekelezaji majukumu yao sambamba na kueleza kwa wananchi namna serikali ya Raisi Samia ilivyofanya kazi kubwa ya kuleta maendeleo kwa wananchi wa mkoa huo.


Mwisho.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI