Header Ads Widget

MWANAFUNZI MWANAHARAKATI WA PALESTINA AKAMATWA KATIKA USAILI WA URAIA WA MAREKANI

 


Mratibu wa maandamano ya wafuasi wa Palestina katika Chuo Kikuu cha Columbia amekamatwa na maafisa wa uhamiaji alipokuwa akifanyiwa usaili kama sehemu ya maombi yake ya uraia wa Marekani, wakili wake anasema.

Mohsen Mahdawi, mwenye kadi ya kijani ambaye anatazamiwa kuhitimu mwezi ujao katika chuo cha New York City, alizuiliwa Jumatatu huko Colchester, Vermont.

Wakili wake alisema Bw Mahdawi aliwekwa kizuizini "kulipiza kisasi moja kwa moja" kwa jukumu lake katika maandamano ya kupinga vita vya Israeli na Gaza.

Wengine walioshiriki katika maandamano ya chuo kikuu kupinga vita, akiwemo Mahmoud Khalil wa Chuo Kikuu cha Columbia na Rumeysa Ozturk wa Chuo Kikuu cha Tufts, wamezuiliwa.

BBC imewasiliana na Uhamiaji na Utekelezaji wa Forodha wa Marekani (ICE) kwa maelezo zaidi kuhusu kesi ya Bw Mahdawi.

Video iliyosambazwa kwenye mitandao ya kijamii inaonekana ikimuonyesha akisindikizwa ndani ya gari na maafisa wawili waliovalia jaketi za polisi.

Wakili wake, Luna Droubi, alisema: "Utawala wa Trump ulimshikilia Mohsen Mahdawi kulipiza kisasi moja kwa moja kwa utetezi wake kwa niaba ya Wapalestina na kwa sababu ya utambulisho wake kama Mpalestina.

"Kuzuiliwa kwake ni jaribio la kuwanyamazisha wale wanaozungumza dhidi ya ukatili wa Gaza. Pia ni kinyume cha katiba."

Wakili huyo aliwasilisha ombi kwa mahakama ya shirikisho kwa ajili ya amri ya zuio la muda ili kuzuia mamlaka ya uhamiaji ya Marekani kumhamisha Bw Mahdawi kutoka Vermont au kumfukuza kutoka Marekani.

Jalada la mahakama linasema kuwa Bw Mahdawi alizaliwa katika kambi ya wakimbizi katika Ukingo wa Magharibi na kuhamia Marekani mwaka wa 2014.

Bw Mahdawi, ambaye amekuwa mkaazi wa kudumu wa Marekani tangu 2015, hajulikani aliko, kulingana na Bi Droubi.

Bw Mahdawi, ambaye alianzisha Jumuiya ya Wanafunzi wa Kipalestina ya Columbia, amekuwa mkosoaji mkubwa wa operesheni ya kijeshi ya Israeli huko Gaza.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI