Header Ads Widget

TANESCO YAWAALIKA WANANCHI KUTEMBELEA BANDA KUPATA ELIMU KWENYE MAONESHO YA OSHA SINGIDA

Na Thobias Mwanakatwe,SINGIDA 

SHIRIKA la Umeme Tanzania (TANESCO) limetoa wito kwa wananchi wa ndani na nje ya Mkoa wa Singida kufika katika banda la maonyesho ya Wiki ya Usalama na Afya yalitoandaliwa na Wakala wa Usalama na Afya Mahala pa Kazi (OSHA) ili waweze kupata elimu namna shirika linavyotoa huduma na linavyozingatia suala la usalama na afya kwa wafanyakazi wake na wananchi kwa ujumla.

Maonyesho hayo ambayo yameanza Aprili 24 na yatahitimisha Aprili 30 mwaka huu ambapo yanafanyika kwenye viwanja vya Maonesho Mandewa Manispaa ya Singida ambayo yanakwenda sambamba na maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Dunian (Mei Mosi) ambayo mwaka huu kitaifa yanafanyika mkoani Singida.



Afisa Afya na Usalama Mahala pa Kazi kutoka TANESCO Makao Makuu, Dativa Mahembe, akizungumza leo na waandishi wa habari amesema suala la afya na usalama ni jukumu la kila mwananchi na mfanyakazi.


"Nitoe wito kwa wananchi usalama ni jukumu la kila mwananchi yaani usalama wako ni jukumu lako iwe kwa mfanyakazi au raia kwa hiyo unapopewa elimu hakikisha unazingatia maana kukitokea tatizo la umeme anayeathirika ni wewe,"amesema Dativa.



Dativa amesema TANESCO imekuwa ikitoa elimu mara kwa mara kupitia kwenye vyombo vya habari,kuwafuata wanafunzi mashuleni na kwa wafanyakazi hiyo imekuwa kama sala kabla ya kuanza kazi wanapewa elimu ili wachukue tahadhari na afya zao kuwa salama.


Amesema pamoja na kwamba wafanyakazi wanalindwa kwa kupatiwa vifaa ambavyo vinawazuia wasipate tatizo la kunaswa na umeme lakini kwa kuwa miundombinu ya umeme imepita kwenye makazi ya wananchi hivyo nao wananchi wanapewa kipaumbele kupewa elimu.

"Kama unavyofahamu wafanyakazi wanapanda kwenye nguzo na kuingia kwenye maeneo ambako ni hatarishi shirika limetengeneza sera ambazo zinatuongoza kuhakikisha wafanyakazi wanakuwa salama kwa kuwapa vifaa kinga,viatu na sare ambazo hata ikitokea tatizo vinawalinda," amesema Dativa.


Aidha, Dativa ametoa wito kwa wananchi kufika katika maonesho hayo ili waweze kupata elimu kutoka kwa wataalam wa TANESCO.


MWISHO

.







 

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI