Header Ads Widget

IKULU YA WHITE HOUSE YAMFUKUZA KAZI MKUU WA SHIRIKA LA USALAMA LA TAIFA



Utawala wa Trump umemfukuza kazi Jenerali Timothy Haugh, mkuu wa Wakala wa Usalama wa Kitaifa na Kamandi ya Mtandaoni ya Marekani, mshirika wa BBC wa Marekani CBS ameripoti.

Haijabainika kwa nini aliondolewa, lakini hatua hii inakuja baada ya mkutano kati ya Rais Donald Trump na mwanaharakati wa mrengo mkali wa kulia Laura Loomer siku ya Jumatano.

Bi Loomer aliripotiwa kumtaka Trump kuwafuta kazi wafanyakazi ambao alishuku kuwa hawakuunga mkono ajenda yake.

Alichapisha kwenye X kwamba Jenerali Haugh na naibu wake Wendy Noble, ambao vyombo vya habari vya Marekani viliripoti pia kwamba wameondolewa, "wamekuwa si waaminifu kwa Rais Trump.

Ndiyo maana wamefukuzwa kazi." Kabla ya kuripotiwa kufutwa kazi kwao, Trump aliwaambia waandishi wa habari kwamba atawaondoa wafanyakazi wowote wanaoonekana kutokuwa waaminifu.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI