Siku ya Ijumaa, China imetangaza itatoza ushuru wa 34% kwa bidhaa zinazoagizwa kutoka Marekani, kuanzia Aprili 10 mwaka huu.
Hatua hiyo ni jibu la ushuru wa Marekani wa asilimia sawa na hiyo kwa bidhaa za China, iliyotangazwa na Rais wa Marekani Donald Trump mapema wiki hii.
Ushuru wa 34% wa Marekani dhidi ya China ni nyongeza ya ushuru uliotangazwa hapo awali, ikimaanisha kuwa kiwango jumla cha ushuru dhidi ya China ni 54%.
Wizara ya Biashara mjini Beijing imesema imefungua kesi kwa Shirika la Biashara Duniani (WTO) kuhusiana na ushuru wa Trump.
China pia imetangaza Ijumaa itaweka vizuizi zaidi vya usafirishaji kwa madini adimu, yanayotumika katika bidhaa kama vile chipu za kompyuta na betri za EV.
0 Comments