Header Ads Widget

DUNIA YAPATA PIGO KIFO CHA PAPA FRANCIS " DR.MUKAMA

 


Na Shomari binda-Matukio Daima

KADA wa Chama cha Mapinduzi ( CCM)Dr.Wilson Mukama amesema dunia imepata pigo kufuatia kifo cha kiongozi wa Kanisa Katoriki Duniani Papa Francis.


Akizungumzia kifo hicho kilichotokea leo aprili 21 akiwa na umri wa miaka 88 kuwa ni pigo kubwa.

Dr.Mukama amesema kiongozi huyo wa kiroho alikuwa mpatanishi na Mara kadhaa amekuwa akihubiri amani

" Ni kiongozi mkubwa wa kiroho ambaye dunia imepata pigo kwa kuwa alikuwa mpatanishi na aliyehubiri amani.

" Natoa pole kwa waumini wote wa Kanisa Katoriki hapa nchini na duniani kote kufuatia kifo hiki",amesema Dr.Mukama

Vatikani imethibitisha kifo chake Jumatatu ya Pasaka, tarehe 21 Aprili 2025, kufuatia kuugua kwa muda mrefu kutokana na nimonia.

Papa alizaliwa kama Jorge Mario Bergoglio na aliingia kwenye historia mwaka 2013 kama Papa wa kwanza kutoka Amerika ya Kusini na Myesuiti wa kwanza na wa kwanza kutoka nje ya Ulaya baada ya karne nyingi.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI