Mkurugenzi wa kampuni ya Rock Solution alipokuwa akizungumza na baadhi ya walezi wa kituo cha kulelea watoto Wilaya Kahama
NA CHAUSIKU SAID
MATUKIO DAIMA MEDIA MWANZA
Mkurugenzi wa Rock Solution Zacharia Nzuki ameeleza kuwa yuko tayari kuhakikisha anawahudumia watoto yatima na wanaoishi katika mazingira magumu ili kuhakikisha wanapata furaha.
Hayo ameyabainisha Jana katika sherehe ya pasaka aliposhiriki chakula Cha pamoja na watoto kutoka kituo cha Mvuma senta, peace pamoja na New hope Wilaya ya Kahama Mkoani Mwanza, na kueleza kuwa watoto wanachangamoto nyingi hivyo jamii inapaswa kuwashika mkono ili waweze kuwa katika mazingira sana.
Nzuki amesema kuwa watanzania wametakiwa wakuwa na mila desturi ya kuwakumbuka watoto yatima na wanaoishi katika mazingira magumu kwa kuwapa mahitaji maalumu yatakayowasidia katika vituo vyao wanavyolelewa na sio kuwaacha wakiishi katika mazingira magumu.
“kama tungesema jamii iwachukue watoto hawa na vituo visiwepo na maandiko ya kibublia yanatueleza kuwa ya kama tu ataishi na Mtoto yatima au mazingira magumu Mtoto huyo anapaswa kupewa kipaumbele katika kuhudumiwa tofauti na watoto wengine sidhani kama Kuna mtu angeweza kufanya hivyo Kwa ajili ya kubarikiwa"Alisema Nzuki.
Amefafanua kuwa hakuna jambo ambalo ni gumu kwa watanzania kama kutoa sadaka liwe katika swala la kiimani au katika kuwasidia watoto yatima au wanaoishi katika mazingira magumu jambo ambalo watu wengi wamekuwa wakishindwa kulitekeleza ipaswavyo na kuwaachia kikundi cha watu wachache huku wengine wakiwa na uwezo wa kuwahudumia watoto hao.
Kwa upande wake mchungaji wa kanisa la bethali Assembly of God peter Mpega ameeleza ameeleza kuwa watanzania Wana mila na desturi ya kutotoa na kuzoea kupokea misaada kutoka kwa wazungu wakati hata na wao wanauwezo wa kutoa.
"tunamezoea kupokea misaada kutoka kwa wazungu wakati uwezo wa kujihudumia wenyewe tunao Katika jamii zetu, kuna watoto wengi wanaokua katika mazingira magumu—wengine ni yatima waliopoteza wazazi wao, na wanaishi katika hali ya uhitaji mkubwa, wakikosa huduma muhimu kama chakula, mavazi, elimu na matunzo ya afya kuwa moyo wa zacharia anatamani watoto kuishi kama wafalme na kula vizuri" Alisema mchungaji peter.
Baraka james ni mmoja wa vijana wanaolelewa katika vituo hivyo amemshukru mkurugenzi wa rock solution kuendelea kuwakumbuka kila wanapokuwa na changamoto mbalimbali,na kuwaomba watanzania wengine kujitokeza kuwasidia watoto wanaoishi katika mazingira magumu pamoja na yatima.
“usifurahie kuwaona watoto wanaangaika mtaani wakati mnauwezo wa kuweza kutusaidia pia mnapotusaidia mnatupatia moyo na sisi tunaona tuna jamii inatutazama inatupatia furaha ndani ya mioyo yetu” alisema Baraka.
0 Comments