Header Ads Widget

CHALAMILA: KIONGOZI MWENYE MAONO MAKUBWA YA KIUONGOZI NDANI YA SIASA NA SERIKALI

 


Na Matukio Daima Media 

Albert Chalamila ni mmoja wa viongozi wachache waliodumu kwa muda mrefu katika nyadhifa mbalimbali za kiutendaji serikalini na ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM). 

Ikumbukwe kuwa umaarufu wake umetokana na msimamo wake thabiti, uwezo wa kusimamia sheria, na uthubutu wa kusema ukweli pasipo woga. 

Anaamini katika uwajibikaji, uadilifu, na utendaji wa haraka, sifa ambazo zimemfanya kutambulika kama kiongozi mwenye maono makubwa ya kiuongozi katika siasa na serikali.

Tangu aingie kwenye nafasi ya ukuu wa mkoa mwaka 2018, Chalamila ameonesha dira ya kweli ya uongozi unaolenga maendeleo ya watu.


 Alipoanza kama Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, alijitokeza kwa kuhimiza uwajibikaji miongoni mwa watendaji wa serikali, kudhibiti matumizi mabaya ya fedha za umma, na kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora za kijamii. Alijenga uhusiano wa karibu na jamii, huku akiwahimiza viongozi wa chini kutekeleza majukumu yao kwa weledi.

Chalamila anaamini kuwa uongozi bora hujengwa kwa misingi ya nidhamu, usimamizi makini wa rasilimali, na uwazi. Hii imekuwa dhihirisho katika kila mkoa aliosimamia – kutoka Mbeya, Mwanza, Kagera hadi Dar es Salaam. Katika kila mkoa, ameacha alama ya ufanisi, hasa katika usimamizi wa miradi ya maendeleo, ambapo miradi mingi aliyosimamia imekamilika kwa wakati na kwa viwango vinavyokubalika.

Katika uongozi wake wa sasa kama Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Chalamila ameendelea kuonesha maono ya juu katika kuiongoza mkoa huo mkubwa na changamano. 

Amehimiza matumizi ya teknolojia katika ukusanyaji wa mapato, kupambana na rushwa, pamoja na kuimarisha huduma za kijamii kama afya, elimu na miundombinu.

 Kupitia maono yake ya kuona jiji la Dar es Salaam linakuwa la kisasa na lenye nidhamu, amekuwa mstari wa mbele katika kupiga vita ujenzi holela, utupaji taka kiholela, na biashara zisizo rasmi katika maeneo yasiyostahili.


Chalamila pia ni mwanasiasa aliyebobea ndani ya CCM Amefanya kazi ya kuimarisha chama katika ngazi ya mkoa kwa mkoa wa Iringa Kwa kipindi kifupi ameancha Alama , akijenga misingi ya umoja, mshikamano na maadili ya chama. 

Anaeleweka kama kiongozi anayeheshimu mamlaka ya juu, lakini pia anayethubutu kutoa maoni yake binafsi pale anapoona kuna kasoro za kisera au kiutendaji.

Maono ya Chalamila ni kuona Tanzania inapata viongozi wanaotanguliza maslahi ya wananchi, wanaojituma bila hofu na wanaojitokeza kwa vitendo badala ya maneno tu. 

Hii ndiyo sababu licha ya kukumbana na changamoto mbalimbali, bado amekuwa akipewa nafasi ya kuongoza mikoa tofauti na kuaminiwa na marais waliomtangulia na aliyepo madarakani sasa.


Albert Chalamila ni kiongozi mwenye maono makubwa yanayolenga kuibadilisha Tanzania kuwa taifa lenye maendeleo, nidhamu na uwajibikaji. Ni mfano wa aina ya viongozi wanaohitajika katika nyanja za siasa na serikali kwa sasa na kwa vizazi vijavyo.

Itaendelea ...


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI