Na Matukio Daima Media Zanzibar.
Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo Doroth Semu amesema chama hicho kitashiriki kikamilifu katika uchaguzi mkuu wa mwezi oktoba mwaka huu licha ya baadhi ya vyama kutangaza kutoshiriki uchaguzi huo.
Doroth ameyasema hayo leo April 16 wakati alipokua akizungumza na waandishi wa habari mjini Unguja.
Amesema wameamua kushiriki uchaguzi kuipa thamani kura za wananchi pamoja na kuwepo kwa changamoto nyingi ambazo zimekua zikikandamiza ustawi wa demokrasia Nchini.
Amesema watatumia uchaguzi mkuu 2025 kukabiliana na watawala vyovyote vile watakavokuja lakini hawatafanya kabisa kosa ka kususia.
"Tutaendelea kulinda demokrasia na tupo tayari kupambana na yoyote yule" alisema.
Pamoja na hayo kiongozi huyo wa Chama alisema wameamua kuja na maamuzi hayo baada ya kujifunza kwa kina mataifa yanayosusia uchaguzi na madhara yake.
Aidha amesema watautumia pia uchaguzi huo kama jukwa la mapambano na kulinda demokrasia.
Katika hatua nyengine amesema Chama cha Mapunduzi CCM wameshindwa kuwatoa watanzania walio wengi kwenye dimbwi la umasikini ambao ndio kiu ya walio wengi.
Mwisho
0 Comments