Na Matukio Daima Media,Zanzibar
Mwenyekiti wa Taifa Chama cha ACT Wazalendo. Othman Masoud Othman amesema wamefanya jitihada kubwa kuleta hali ya maridhiano Zanzibar kabla ya kuingia kwenye uchaguzi mkuu mwezi Oktoba mwaka huu kuepusha maafa yasiokua ya lazima lakini wenzao hawakua tayari na hali hiyo.
Othman ambae pia ndie Makamu wa kwanza wa Rais Zanzibar ameyasema hayo kwa nyakati totauti wakati akiendelea na ziara ya umarishaji wa Chama Mkoa wa kusini Unguja leo April 12 baada ya kukamilika kwa ziara kama hiyo kisiwani Pemba.
Amesema wakati wanatafuta suluhisho la changamoto za kisiasa Zanzibar walikutana na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM ambae ni Rais wa Jamuhuri ya Muungano Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan na kukubaliana kwa pamoja mambo kadhaa ambayo yangekua muarubaini na kumaliza kabisa kilio cha muda mrefu kila ufanyikapo uchaguzi mkuu.
"Cha kushangaza zilipoundwa timu za utekelezaji wa maagizo wenzetu wakageuka kuja na mengine mapya wakati hakua muda wa majadiliano tena.
Mwisho
0 Comments