Na Shemsa Mussa -Habari na Matukio App Kagera.
WAZIRI Mkuu wa Jumuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Kassim Majaliwa amesema,Serikali inatambua michango inayotolewa na kanisa katoriki ikiwa ni katika kuunga mkono jitihada za Serikali kwa kutoa huduma mbalimbali za jamii.
Ametoa kauli hiyo leo 19 march 2025 wakati akishiriki maadhimisho ya jubilee ya miaka 25 ya uaskofu wa askofu mstaafu mwasham Methodius Kilaini katika kanisa katoriki Jimbo la Bukoba mkoani Kagera.
Majaliwa amesema,kanisa katoriki limekuwa likitoa huduma kwa jamii ya afya, elimu na Maji kwa kujenga miundombinu mbalimbali ndani ya mkoa wa Kagera.
Amesema, Serikali itaendelea kuungana na makanisa na misiki ikiwa ni katika kuunga juhudi za kutolea huduma za kijamii na kupokea ushauri bila kukiuka misingi ya nchi.
Aidha,MheMajaliwa amesema kwa kutambua hilo kutakuwa na mashirikiano mbalimbali na viongozi wa dini ambapo Serikali kwa sasa inahitaji kurudisha maadili kwa vijana.
Amesema,ipo nguvu kubwa kwa viongozi wa dini katika jamii hasa kupitia mahubili na mawaidha yanayotolewa Moja kwa moja kwenye nyumba za ibada.
"Nguvu ya kiimani katika mahubili na mawaidha ni njia Moja wapi ya kurudisha maadili ya kitanzania yenye utu,haki, na amani ili kujenga nchi"alisema Majaliwa.
Ameongeza kuwa,jamii ndio inayoweza kulinda amani ya nchi kupitia endapo itakuwa na maadili ambayo yatafanyika na kila mmoja aweze kuwa mlinzi wa wengine.
Mkuu wa mkoa wa Kagera Mhe Bi Fatma Mwassa amesema,viongozi wa dini wamekuwa msaada katika ushauri wa masuala ya kiutendaji na uchumi kuunga mkono maendeleo ya mkoa kwa kuanzisha miradi ya wananchi.
Mwassa amesema, michango mikubwa imefanyika katika kuwashirikisha na kuingia katika bidii za afya na vikao vya maendeleo ya mkoa kwa kutoa maarifa na uboreshaji wa mijadala.
"Nimetolea mfano hapa askofu kilaini ambaye alikuwa katika bodi ya hospitali alishauri jinsi ya kusimamia na kutolea huduma ya afya kwa jinsi ambavyo wanafanya katika hispotali za kanisa akiwa kama mzoefu na mwanzishaji wa miradi"alisema Mwassa.
Makamo wa Rais Baraza la maaskofu nchini Eusebius Nzigilwa wa Jimbo katoriki mkoa wa Mpanda alisema askofu mstaafu Kilaini alitumikia Baraza hilo kwa kuunganusha maaskofu mbalimbali.
Amesema, kwa miaka ambayo alitumikia utume wa upadre ikiwa ni miaka 53 amehudumia makanisa ya katoriki maeneo mbalimbali nchini na kuanzisha miradi ya maendeleo akiwa Katibu mkuu katika Baraza .
Amesema, akiwa askofu msaidizi Jimbo katoriki la Bukoba amesimamia miradi ya kanisa na kufanya utume mbalimbali katika makanisa hayo.
KWA HABARI WAKATI WOTE PAKUA APP YETU BOFYA LINK HII
PAKUA APP YA MATUKIO DAIMA MEDIA ILI KUPATA HABARI ZETU KWA WAKATI ZAIDI
0 Comments