Na Gabriel Kilamlya Matukio DaimaAPP NJOMBE
Waziri mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa Majaliwa,ameziagiza taasisi na Mamlaka zote zinazohusika na uhifadhi wa misitu kuhakikisha zinaongeza nguvu katika uhifadhi wa mazingira ili kuokoa zaidi ya hekta laki nne zinazopotea.
Waziri mkuu Majaliwa ametoa agizo hilo mkoani Njombe wakati akifunga maadhimisho ya misitu Duniani ambapo amesema bila ya uhifadhi mazingira,Taifa litaendelea kupata hasara kubwa kwa kuharibiwa na misitu.
Awali Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Dokta Pindi Hazara Chana,amesema kuwa nusu ya Tanzania ni Misitu hivyo serikali itaendelea kuilinda na kuhifadhi misitu kwani ni rasimali muhimu kwa taifa.
Mkuu wa mkoa wa Njombe Antoni Mtaka amesema kuwa mkoa wa Njombe kwa miaka 3 umepata hasara ya zaidi ya shilingi bilioni 200 kutokana na moto kuunguza miti ya baadhi ya wakulima.
Jasel Mwamwala na Scolastika Kevela mwenyekiti wa UWT mkoa wa Njombe wameeleza namna ambavyo wananchi wamenufaika kupitia maadhimisho haya kufanyika mkoani hapa.
Kauli mbiu ya kitaifa mwaka huu ni "Ongeza thamani ya mazao ya misitu kwa uendelevu wa rasilimali kwa kizazi hiki na kijacho".
0 Comments