Header Ads Widget

CHONGOLO AFUNGUKA FEDHA ZA SAMIA SONGWE, AKOSHWA NA HATUA YA KUSAINI MKATABA WA MAJI.

 


Na Moses Ng'wat, Tunduma.


Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Daniel Chongolo, amesema hatua ya kusainiwa kwa mkataba wa Mradi wa Maji wa Tunduma-Vwawa ni jambo kubwa linalothibitisha dhamira ya dhati ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kuboresha maisha ya Watanzania, hususan wakazi wa Songwe.



Akizungumza katika hafla ya utiaji saini wa mkataba huo, Machi 20, 2025, Chongolo aliipongeza Serikali ya Awamu ya Sita kwa kuendelea kuwekeza kwenye miradi mikubwa ya kimkakati, akisema hatua ya kusaini kwa mkataba huo wenye thamani ya shilingi biliini 119.95 ni ushahidi na dhamira ya wazi juu upendo wake kwa wananchi wa Songwe.



"Ndugu zangu wana Songwe, tunapaswa kumshukuru sana Mheshimiwa Rais kwa upendo wake mkubwa kwetu kama mjuavyo Tanzania ni nchi kubwa, lakini ndani ya miaka minne ya uongozi wake, Songwe imepokea zaidi ya shilingi trilioni moja kwa ajili ya kushughilika na changamoto za wananchi," alisema Chongolo huku akishangiliwa na wananchi.


Alisema kusainiwa kwa mkataba huo wenye thamani ya shilingi Bilioni 119.95 kutasaidia  kuboresha upatikanaji wa huduma ya Maji kwa wakazi wa miji ya  Tunduma, Vwawa na Mlowo ndani ya mkoa wa Songwe



Katika hafla hiyo  iliyofanyika kwenye Uwanja wa Shule ya Msingi Tunduma, mgeni rasmi alikuwa Waziri wa Fedha, Dkt. Mwigulu Nchemba (Mb), ambaye alishuhudia utiaji saini wa mkataba kati ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji, Mhandisi Mwajuma Waziri, kwa niaba ya Serikali, na Meneja Mradi wa Kampuni ya China Civil Engineering Construction Corporation (CCECC), Bw. Ning Yunfeng.



Aidha, Mkuu wa Mkoa wa Songwe aliwashukuru viongozi wa Wizara ya Maji wakiongozwa na Waziri Mheshimiwa Juma Aweso pamoja na Katibu Mkuu Mhandisi Mwajuma Waziri kwa usimamizi wao mzuri wa miradi ya maji nchini.


Mradi huo unatarajiwa kuanza kutekelezwa mara moja, huku Serikali ikiahidi kufuatilia kwa karibu kuhakikisha unakamilika kwa wakati na kwa viwango bora, ili wananchi wa Songwe waondokane na adha ya uhaba wa maji.


Mwisho.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI