Na SHAMILA RAJAB MATUKIO DAIMA MEDIA
Kada wa Chama cha mapinduzi CCM wilaya ya Kilolo mkoani Iringa Shamd Nzogela amewataka wanawake wa mkoani humo kuweza kujitokeza kwa wingi kuunga mkono jitihada zinazofanywa na Dkt Samia Suluhu Hassan hii ikwemo kujitokeza kwa wingi katika kujiandikisha katika dafrati la kupiga kura ili kuendeleza kijivunia kazi zinazofanywa na Dkt Samia Suluhu Hassan.
Akizungumza hii leo katika kipindi cha mjadala magazetini kinachorushwa na Matukio Daima tv Nzogela amesema pongezi kubwa zimuendee Dkt Samia Suluh Hassan kwa mafanikio makubwa ya utendaji kazi wake ambayo yamekuwa yakisaidia jamii kwa kiasi kikubwa huku akiwataka wanawake kujitokeza kuunga mkono juhudi za Rais Dkt. Samia Suluhu.
''katika kuelekea siku ya wanawake duniani mimi nilikuwa nawaomba wanawakwe waweze kujitokeza kwa wingi katika kuhakikisha wanaunga mkono kazi na juhudi ambazo zimekuwa zikifanywa na Rais ili kumtia moyo aweze kuendelea kufanya kazi kwa nguvu zote lakini pia wajiandikishe katika daftari la kudumu la kupiga kura ili waweze kumpa Mama nafasi nyingine tena''
Katika hatua nyingine Kada huyo ameeleza kujivunia na ujenzi wa hospitali ya wilaya ya Kilolo ambayo imesaidia kupunguza vifo vya mama na mtoto jambo linalosaidia maendeleo katika sekta ya afya katika mkoa wa Iringa ametoa pongezi zake za dhati kwa Dkt Samia Suluhu Hasssan kwa kile anachoendelea kukifanya katika jamii.
'' kabla ya ujenzi wa kituo hiki cha afya kumekuwa na changamoto ya vifo vya mama na mtoto ambavyo vimekuwa vikizua hofu na mashaka makubwa kwa jamii na hii ilikuwa inatokana na ubovu wa miundombinu ya barabara lakini pia umbali wa vituo vya afya jambo lililokuwa linapelekea hatari kwa maisha ya mama na mtoto''
Nzogela ameeleza kuwa takwimu za awali zilionesha kwamba wanawake wajawazito na watoto wachanga walikuwa hatarini zaidi kutokana na ukosefu wa huduma bora za uzazi na uhaba wa wataalamu wa afya hata hivyo kupitia juhudi za serikali na uongozi imara wa Dkt Samia,hospitali ya wilaya ya kilolo imeleta mageuzi makubwa katika huduma za afya ya uzazi.
Pia ameeleza kuwa Dkt Samia ameweza kuonesha mafanikio makubwa katika kusimamia utoaji wa huduma bora kwa wanachi na ni jukumu letu sote wanajamii kuhakikisha kuwa tunamuunga mkono Rais wetu kwa juhudi hizi ambazo amekuwa akizifanya hii ni kuhakikisha kuwa tunatunza vizuri miundombinu yetu na kutunza afya zetu.
0 Comments