Header Ads Widget

VIFO VYA MAMA NA MTOTO MBIONI KUPOTEA WILAYANI KILOLO TUMUUNGE MKONO RAIS SAMIA -NZOGELA

 

Na Shamila Rajab Matukio Daima Media 

Kada wa Chama cha mapinduzi CCM wilaya ya Kilolo mkoani Iringa Shamd Nzogela ameeleza kujivunia ujenzi wa hospitali ya wilaya ya Kilolo ambayo imesaidia kupunguza vifo vya mama na mtoto jambo linalosaidia maendeleo katika sekta ya afya katika mkoa wa iringa.

Akizungumza hii leo  katika kipindi  cha mjadala magazetini kinachorushwa na Matukio Daima tv Nzogela amesema pongezi kubwa zimuendee Dkt Samia Suluhu Hassan  kwa mafanikio makubwa ya utendaji kazi wake ambayo yamekuwa yakisaidia  jamii kwa kiasi kikubwa.

''kwa miongo kadhaa changamoto ya vifo vya mama na mtoto vimekuwa vikizua hofu na mashaka makubwa kwa jamii na hii ilikuwa inatokana na ubovu wa miundombinu ya barabara lakini pia umbali wa vituo vya afya jambo lililokuwa linapelekea hatari kwa maisha ya mama na mtoto'' 

Nzogela ameeleza kuwa takwimu za awali zilionesha kwamba wanawake wajawazito na watoto wachanga walikuwa hatarini zaidi kutokana na ukosefu wa huduma bora za uzazi na uhaba wa wataalamu wa afya hata hivyo kupitia juhudi za serikali na uongozi imara wa Dkt Samia,hospitali ya wilaya ya kilolo imeleta mageuzi makubwa katika huduma za afya ya uzazi.


''Serikali ya Dkt, Samia imetoa fedha za kutosha kuhakikisha hospitali hii inakuwa na wodi za kisasa za wazazi,chumba cha upasuaji kilicho na vifaa vya kisasa pamoja na vitanda vya kutosha kwaajili ya kina mama wanaojifungua''


Katika hatua nyingine Kada huyo wa CCM ametoa pongezi za dhati kwa serikali ya awamu ya sita ya Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kujali afya za wananchi na kuwekeza katika sekta ya afya.

''Dkt Samia ameweza kuonesha mafanikio makubwa katika kusimamia utoaji wa huduma bora kwa wanachi na ni jukumu letu sote wanajamii kuhakikisha kuwa tunamuunga mkono Rais wetu kwa juhudi hizi ambazo amekuwa akizifanya hii ni kuhakikisha kuwa tunatunza vizuri miundombinu yetu na kutunza afya zetu''

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI