Na Shomari Binda-Musoma Matukio Daima App
WANAWAKE wa jimbo la Musoma vijijini wamemshukuru mbunge wa jimbo hilo Profesa Sospeter Muhongo kwa jitihada zake za kuhakikisha wanapata huduma bora za afya.
Shukurani hizo wamezitoa mbele ya Mkuu wa Wilaya ya Musoma Juma Chikoka machi 6/2025 alipokuwa akifungua kituo cha afya cha Kijiji cha Makojo.
Wamesema wanatambua uhamasishaji na ufatiliaji wa miradi mbalimbali ikiwemo ya afya ambayo inapelekea kuipata na kuwafikia.
Mmoja wa wananchi wa Kijiji hicho aliye shuhudia uzinduzi huo Mwajuma Magoti amesema kituo hicho cha afya kitawasaidia kutotembea umbali mrefu kutafuta huduma za afya hasa za uzazi.
Amesema jitihada za mbunge,nguvu za wananchi na fedha kutoka serikali kuu kwa pamoja zinapelekea kupata huduma.
" Mbunge ambaye ni mwakilishi wetu tunamshukuru sana maana kituo hiki cha afya amekuwa muhamasishaji kuanzia ujenzi wa msingi na leo kimefunguliwa.
" Sana tunamshukuru Mama yetu Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kutuletea fedha nyingi tunaona miradi mingi ikiwemo ya afya",amesema.
Kituo kipya cha afya cha Kata ya Makojo chenye Vijiji 3 vya Chimati, Chitare na Makojo kimezinduliwa na Mkuu wa Wilaya ya Musoma Juma Chikoka huku waganga na wauguzi wakitakiwa kutoa huduma bora kwa wananchi.
Chikoka amesema watoa huduma wanapaswa kuzingatia maadili ya utoaji huduma nzuri kwa wananchi kuanzia kwenye zahanati,vituo vya afya na hospital.
Amesema sio vyema kuona wananchi wakilalamikia huduma wakati serikali imejenga kituo cha afya na kupeleka vifaa tiba na dawa.
Kwa upande wa taarifa iliyotolewa machi 7 2025 na ofisi ya mbunge wa jimbo la Musoma vijijini Profesa Sospeter Muhongo imesema jimbo hilo licha ya kuwa na zahanati na vituo vya afya ina hospital ya Halmashauri yenye vifaa vya kisasa vya matibabu ikiwemo complete radiology unit (mobile digital X-ray),static X-ray), oxygen-production plant, na two ultrasound machines.
Vituo 6 vya afya vilivyopo vikiwa na vifaa tiba vya kisasa ni pamoja na Bugwema, Kiriba, Kisiwa cha Rukuba, Makojo, Mugango na Murangi
Kwa mujibu wa taarifa hiyo zahanati 26 za Serikali na 4 za binafsi zipo zinatoa huduma wakati zahanati 17 mpya zinajengwa kwa nguvu za wananchi na nyingine zimeanza kupokea misaada ya kifedha kutoka serikalini.
" Magari ya wagonjwa 7 likiwemo gari kubwa la kisasa kutoka Japan (lenye vifaa vya upasuaji) ambalo liko kwenye kituo cha afya cha Murangi yanatoa huduma
"Ambulances 7 zipo
(Kwikonero (Hospitali ya Halmashauri),Masinono (Kata ya Bugwema), Kurugee (Kata ya Bukumi)
,Murangi (Kata ya Murangi),Rusoli (Kata ya Rusoli),Nyang'oma (Kata ya Mugango)na Nyasurura (Kata ya Ifulifu)" imesema taarifa hiyo.
Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini Profesa Sospeter Muhongo alitoa Ambulances tano (5) kati ya hizo saba (7) zilizoko jimboni
0 Comments