Header Ads Widget

WANAWAKE WA TANAPA WASHIRIKI KILELE CHA MAADHIMISHO YA WANAWAKE DUNIANI, KITAIFA ARUSHA



Wanawake kutoka Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) wamejitokeza kushiriki katika Kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani, ambayo Kitaifa yanafanyika leo Machi 8, 2025 katika viwanja vya Sheikh Amri Abeid vilivyoko jijini Arusha ambapo Mgeni Rasmi katika maadhimisho hayo ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Maadhimisho hayo yamelenga kutambua na kuenzi mchango wa wanawake katika nyanja mbalimbali kwenye jamii, ikiwemo sekta ya uhifadhi na utalii, ambazo zimekuwa na athari kubwa kwa maendeleo ya Taifa letu.

Katika tukio hili la kihistoria, wanawake kutoka Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) wameungana na wanawake kutoka maeneo mengine nchini kusherehekea siku hii muhimu kwa kutoa elimu ya uhifadhi na utalii kwa jamii ili kujenga jamii yenye uelewa mpana kuhusu masuala ya uhifadhi wa rasilimali za Taifa.

Aidha, ushiriki wa wanawake kutoka TANAPA umelenga pia kuonesha  juhudi zao katika kusimamia, kulinda na kutunza rasilimali za Taifa ambazo zimekuwa na matokeo chanya kiuchumi na kijamii, pamoja na kubadilisha mtazamo wa jamii kuhusu nafasi ya mwanamke katika sekta ya uhifadhi na utalii.








Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI