Wananchi Mkoani Kagera wameombwa kujitokeza katika ujio wa Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapindizi Tanzania Bara na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Tanzania Mhe Stephen Wasira.
Akizungumza na wananchi kupitia vyombo vya habari Katibu wa siasa na uenezi Mkoa,Ndg Hamimu Mahmudu Omary amesema kiongozi huyo anatarajiwa kuingia Mkoani Kagera Tarehe 22march 2025 na atafanya ziara kwa siku 3.
"Tutampokea Mhe Wasira Tarehe 22march katika uwanja Wetu wa ndege hapa Bukoba na baada ya hapo atakuja ofisini kwa ajili ya kusaini na baadae ataelekea Bukoba vijijini katika kata ya kemondo kwa ajili ya kuzungumza na wananchi atawasikiliza na kutatua kero mbalimbali, amesema Ndg Hamimu".
Aidha,Ndg Hamimu ameongeza kuwa katika ziara hiyo ya Mhe Wasira atakwenda Wilayani Karagwe tarehe 23march ambapo atafanya kikao Cha ndani na baadae atazungumza na wananchi katika eneo Hilo na siku ya 24march Mhe wasira atakwenda wilaya ya Ngara pia atafanya mkutano na wananchi na baada ya hapo atahitimisha ziara yake Tarehe 25 Ndani ya Manispaa ya Bukoba.
Pia Hamimu ameeleza kuwa lengo la ziara hiyo ni kuimalisha chama Cha Mapinduzi CCM na kuzungumza na wanachama wote kwani ni ziara yake ya kwanza tangu apate wadhifa huo wa kuwa Makamu Mwenyekiti Tanzania Bara ,pia amesema kupitia Mikutano ya hadhara atakayoifanya atafuatilia vyema utekelezaji wa ilani ya Uchaguzi ya chama hicho na atasikiliza kero mbalimbali zinazowakabili wananchi wa Mkoa huo na kuzipatia ufumbuzi.
Ametoa rai kwa wananchi wote wa Mkoa kagera kujitokeza kwa wingi na kuhudhulia katika Kila hatua zote za ziara hiyo ikiwemo siku ya mapokezi katika uwanja wa Ndege Bukoba Tarehe 22march 2025 majira ya Saa 5 asubuhi.
0 Comments