Header Ads Widget

POLISI MOROGORO YAWASHIKILIA WATATU TUHUMA ZA WIZI WA MAFUTA

 


JESHI la Polisi Mkoani Morogoro linawashikilia mameneja watatu wa Vituo vya mafuta vya Simba Oil na kumsaka dereva wa kampuni ya mafuta ya Meru kwa tuhuma za kula njama na kuiba mafuta ya Dizel lita 35,700 yaliyokuwa yakisafirishwa kwenda  Lubumbashi nchini DRC Congo kisha kuchoma Lori hilo.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro SACP Alex Mkama alithibitisha tukio hilo kutokea Usiku wa kuamkia Machi  16 mwaka huu katika maeneo ya barabara ya Iringa .

Alisema dereva wa Lori la mafuta Abubakar Mwichangwe mkazi wa Jijini Dar es salaam akiendesha Lori lenye namba za USAJILI T 661 Bxb likikokota tela namba T 489 BHC aina ya Fao  akitoka Dar es salaam kwenda Lubumbashi alishusha mafuta kwenye Vituo vya Simba Oil kisha kujifanya amepata ajali.


Mkama alisema dereva huyo kwa kushirikiana na mameneja hao watatu wa Simba Oil hao aliowataja kuwa ni Hamidu Said (50) meneja mkuu mwenye makazi yake Jijini Dar es salaam, Abiner Mohamed (25) meneja wa kituo Cha Mkambalani na Abdallah Nihedi (30) meneja wa kituo cha Morogoro waliiba mafuta hayo aina ya Dizel lita 35,700 ya thamani ya shilingi milioni 77.

Akaongeza kuwa Dereva  huyo ambaye ametoweka na Polisi inaendelea kumsaka alikula njama na kuiba mafuta ya Dizel aliyokuwa akiyasafirisha kwenda Lubumbashi.

"alikwenda kuyashusha mafuta aliyokuwa akiyasafirisha kwenda nje kwenye Vituo vya mafuta vya Simba Oil vya Mkambalani Morogoro na Morogoro ambalo kituo kimoja alishusha lita 10,000 na kwingine lita 25,700 na kisha akaenda kutengeneza ajali"Alisema Kamanda Mkama.

Mkama Alisema Dereva Mwichangwe aliendesha Lori hilo na tela lake vikiwa havina mafuta hadi eneo la Misufini katika Kijiji cha Msimba ambapo aliliingiza gari hilo korongoni na kulichoma moto Ili kuaminisha uma kuwa amepata ajali.

Akasema uchunguzi zaidi wa tukio hilo bado unaendelea ingawa akawaonya madereva kuacha tamaa ya kupata Mali kwa njia zisizo sahihi.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI