Header Ads Widget

TMDA YAJIVUNIA MIAKA MINNE YA RAIS SAMIA KWA KUTOA GAWIO LA BILIONI 23.3


Na. Andrew Chale, Matukio Daima App.

MAMLAKA ya Dawa na Vifaa tiba nchini (TMDA) katika kipindi cha miaka minne (4) Madarakani ya Mhe. Samia Suluhu Hassan wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, imetekeleza majukumu yake mbalimbali ikiwemo kutoa gawio kwa Serikali kiasi cha Tsh.23.3 Bilioni na mafanikio mengine kadha wa kadha.

Kwa mujibu wa taarifa kwa Umma, leo Machi 19,2025. TMDA imepongeza namna bora ya Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Mhe. Samia huku ikiainisha mafanikio mbalimbali.

Baadhi ya mafanikio hayo ni pamoja na:

Usajili wa viwanda 18 vya dawa, huku viwanda  140 vya vifaa tiba na vitendanishi na hivyo kuchangia katika Uwekezaji.

Kusajili zaidi ya bidhaa 8,303 za dawa na 3,019 za vifaa tiba na vitendanishi baada ya kujiridhisha na ubora, usalama na ufanisi wake.

"Kuongeza bajeti kulikowezesha utoaji huduma kwa ufanisi na kutoa gawio kwa Serikali kiasi cha Tsh. Bilioni 23.3.

Lakini pia Uwekezaji wa bilioni 15 katika ununuzi wa vifaa vya kisasa vya maabara ili kuwezesha kufanya maamuzi ya kisayansi.

Matumizi ya mifumo ya kieletroniki katika huduma za utoaji vibali ambapo sasa vinatolewa ndani ya saa 24.


TMDA pia imeendelea kushikilia cheti cha Ithibati cha ISO 9001:2015 na Ithibati ya Maabara kwa kiwango cha ISO /IEC 17025:2017 katika utoaji huduma bora. Aidha Maabara ya TMDA inatambuliwa na Shirika la Afya Duniani." Imebainisha taarifa hiyo.

Pia Asilimia 98% ya bidhaa kukidhi vigezo vya ubora na ufanisi na hivyo kuhakikisha usalama wa bidhaa za dawa na vifaa tiba katika soko.



Lakini pia, Ongezeko la vituo vya maabara hamishika kutoka 19 hadi 28 ili kuimarisha zoezi la uchunguzi wa sampuli.

Kukamilika kwa ujenzi wa miundombinu ya tanuru la kuteketeza bidhaa zisizofaa eneo la Nala mkoani Dodoma ili kuhakikisha bidhaa katika soko ni zile tu zenye ubora, usalama na ufanisi.

Aidha, Ongezeko la wafanyakazi kutoka 278 hadi 421 na hivyo kuongeza fursa ya ajira nchini.

"Ongezeko la vituo vya ufuatiliaji wa maudhi ya dawa na chanjo hadi kufikia 30 ili kuimarisha ufuatiliaji wa usalama wa dawa na chanjo nchini.

Upanuzi wa ofisi kwa kuongeza sakafu tatu (3) kwenye jengo la ofisi ya Makao Makuu Dodoma." Imebainisha taarifa hiyo.



Baadhi ya Watumishi wa TMDA katika Maabara ya kisasa nchini 





Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI