Header Ads Widget

WADAU WA ELIMU WAALIKWA MUSOMA VIJIJINI MAJADILIANO UBORESHAJI WA ELIMU KWA WANAFUNZI

 

Na Shomari Binda-Musoma 

WADAU wa elimu katika jimbo la Musoma vijijini wamealikwa kwenye majadiliano ( Dialouge)yenye mapendekezo ya uboreshaji,ufundishaji na uelewa wa wanafunzi.

Mualiko huo umetolewa na mbunge wa jimbo la Musoma vijijini Profesa Sospeter Muhongo majadiliano yatakayojadiliwa kwa siku tatu kuanzia machi 25 hadi 27,2025.

Akizungumza na Matukio Daima machi 19,2025 mbunge huyo amesema majadiliano hayo yataongozwa na waadhiri kutoka Chuo Kikuu cha Dar es salam Dr.Zabron Kengera na Dr.George Kahangwa pamoja na mbunifu wa elimu Japhet Makongo.

Amesema majadiliano hayo yana umuhimu mkubwa katika mabadiliko yaliyopo ya mfumo wa elimu hapa nchini hivyo kila muhusika anapaswa kushiriki.

Mbunge huyo amesema majadiliano katika siku ya kwanza tarehe 25 yatafanyika ukumbi wa Kanisa Katoliki Mugango kuanzia saa 3 asubuhi hadi saa 6 kwa kuwashirikisha walimu wa taaluma wa shule za msingi na sekondari wa shule zote ndani ya jimbo hilo.


Katika siku hiyo kuanzia saa 8 mchana hadi saa 11 jioni majadiliano yataendelea kwa kuwashirikisha viongozi wakiwemo viongozi wa Kata wakiwemo watendaji wa Kata( WEO) pamoja na maafisa elimu Kata.

Amesema katika siku ya pili machi 26 majadiliano yataendelea kuanzia saa 3 asubuhi hadi saa 6 kwa kuwashirikisha walimu. wakuu na wakuu wa shule za msingi na sekondari

Aidha mbunge Muhongo amesema siku ya mwisho machi 27 itatumika kwaajili ya mapendekezo kuwasilishwa ambapo mkuu wa Wilaya ya Musoma Juma Chikoka atakuwa mgeni rasmi huku mkurugenzi wa halmashauri na maafisa elimu msingi na sekondari wakiwa washiriki pamoja na madiwani na mbunge mwenyewe.

             

Baada ya shughuli hiyo zawadi zitatolewa kwa waliofanya vizuri kwa mwaka 2024 kama motisha ambapo walimu wa shule zote wamealikwa viongozi,viongozi wa Kata na vijiji pamoja na madiwani

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI