Header Ads Widget

UMOJA WA WANAWAKE HOSPITALI YA RUFAA YA KANDA MBEYA WAPONGEZWA


 Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya, Dkt. Godlove Mbwanji, ameshukuru na kuwapongeza wanachama wa Umoja wa Wanawake wa Hospitali hiyo kwa kuendelea kutoa michango ya sadaka na zawadi kwa ajili ya kuboresha huduma za afya, hususan kwa watoto wa nyanda za juu kusini.  

Akitoa shukrani hizo wakati akipokea kwenye hafla ya makabidhiano ya mashine 5 za kisasa za ‘Neonatal Resucistaires’ zenye thamani ya shilingi milioni 62.5, kwa ajili ya kuongeza uwezo wa kuhudumia watoto wachanga waliozaliwa na changamoto mbalimbali katika kuokoa maisha kwenye sherehe za Siku ya Wanawake Duniani ambayo yalifanyika katika viwanja vya hospitali -meta

Dkt. Godlove Mbwanji Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya amesema “ Ni wapongeze sana sana sana na kuwashukurini muendelezo wa sadaka na zawadi ambazo mmeendelea kutoa kwa hospitali kwa sababu tunafahamu bila kutoa hata kitu chochote utumishi wenu pekee ni sadaka kubwa sana.

Lakini mmeona haitoshi mkaamua kuingia mifukoni kwenu na kutoa zawadi hii kubwa sana kwaajili ya Watoto wetu wa nyanda za juu kusini na hii ni kuunga mkono Jitihada kubwa za Serikali yetu ambayo tumekua tukiona kwa macho yetu katika kuwekeza katika sekta ya afya.” Amesema Dkt. Mbwanji

Dkt. Mbwanji amewaeleza umoja huo wa wanawake kama muhimili mkubwa sana wa afya za wananchi mchango wao ni mkubwa sana na na kuendelea kuwawashukuru.

Nae Mkurugenzi wa Utawala na Huduma Shirikishi wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya Bi Miriam Msalale ameeleza fedha hizo zimepatikana kutokana na michango, inayotokana na posho zao, pamoja na michango ya watumishi wengine na wadau wengine.

“Tumeweza kukusanya kiasi cha shilingi milioni sitini na mbili na laki tano ambazo tumenunua mashine kwaajili ya kuokoa maisha ya watoto wachanga. Tunashukuru Mungu tumeweza kuzikabithi mashine hizi tano.”

Amefafanua kwa pia wamefanya hivyo kwajili ya kuunga mkono, jitihada zinazo onyeshwa na Rais Dr. Samia Suluhu Hassan katika kuinua sekta ya afya, kwa kua amejenga majengo, ameweka miundo mbinu mbali mbali zikiwemo na mashine. Hivyo wao umoja wa wanawake wa hospitali ya Kanda ya Rufa Mbeya, wameona wamuunge mkono kwa kutowa zawadi ya mashine hizo ambazo wanaiamini zinakuenda kuokoa maisha ya watoto wa Changa

Nae Joyce Komba, Katibu wa umoja wa Wanawake Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya akasoma risala ameeleza kuwa Umoja wanawake MZRH Women Group una jumla ya wananchama 671 na ulianza rasmi mwaka 2022 kwa jumla na wanawake hapo awali 400 na hadi hapa kufikia mwaka huu tumekua na ongezeko la wana umoja 271. 

“Kama watumishi wanawake kutoka Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya, tunaungana na wanawake wenzetu katika kuhadhimisha siku hii muhimu na katika maadhimisho ya mwaka 2025, Tuliona busara kurudisha fadhila kwa jamii CSR kwa kununuwa meza 5 za kuhuisha watoto wachanga, zina thamani ya shilingi milioni 62,500,000/=. 

Wao hili lilikujia ili kuhunga mkono jitiada za mama yetu Rais wa awamu hya 6 Daktari Samia Suluh Hassan katika kupunguza vifo vya wajawazito na watoto wachanga ikiwa pamoja na kugusa jamii kubwa wa Tanzania na nchi za jirani tunazopakana nasiambao wanapata matibabu katika hospitali hii. “ Ameeleza Bi. Joyce Komba





Mwisho.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI