Header Ads Widget

UKARABATI MELI YA MV LIEMBA KIZUNGUMKUTI

 


Na Fadhili Abdallah,Kigoma

Kamati ya siasa ya halmashauri kuu ya CCM mkoa Kigoma imesikitishwa na kuchelewa kuanza kwa ukarabati mkubwa wa meli ya Mv.Liemba kwa Zaidi ya miezi sita sasa hivyo wametoa maelekezo kuhakikisha ukarabati huo unaanza haraka.

Mwenyekiti wa CCM mkoa Kigoma, Jamal Tamim alitoa maelekezo hayo wakati kamati hiyo ilipofanyika ziara katika bandari ya Kigoma kutembelea na kukagua maendeeo ya ukarabati wa meli ya abiria na mizigo ya Mv. Liemba na meli yya mafuta Mt Sangara.

Tamim alisema kuwa taarifa ya wasimamizi wa mradi huo Kampuni ya meli Tanzania (TASHICO) kuonyesha ukarabati huo umefanyika kwa asilimia 10 tangu mwezi Julai mwaka jana zinatia simanzi  kwani nguvu kubwa waliyokuwa wanatumia kuwaeleza wananchi kuwa ukarabati huo utafanyika na kumaliza haraka na meli itaanza kutoa huduma muda si mrefu unawafanya kuonekana waongo kwa wananchi.





Kwa upande wake Mbunge wa jimbo la Kigoma Mjini, Kilumbe Ng’enda alisema kuwa jambo la kusikitisha ni kwamba wanaosimamia ukarabati huo wanaeleza tatizo ni cherezo lakini baada ya cherezo kukarabatiwa na kuanza kutoa huduma zimekuwa zikipandishwa meli nyingine za watu binafsi na meli hiyo ikiwa imeachwa pembeni kwa muda mrefu bila kufuata muda wa  mkataba wa ukarabati wa meli hiyo.

Awali Meneja wa tawi la Kigoma wa Kampuni ya meli Tanzania (TASHICO), Humphrey Mwambungu alisema kuwa tayari ukarabati wa meli hiyo umeanza kwa kuondoa injini na mashine zilizopo ndani ya meli ili kuweka mpya na kwamba mu si mrefu itapandishwa kwenye cherezo ili kufanyiwa ukarabati wa nje sambamba na ukarabati wa ndani kuendelea.

Mwambungu alisema kuwa awali meli ya MT Sangara ndiyo ilikuwa inakarabatiwa ikiwa juu ya cherezo na tayari imeshashushwa ikiendelea na umaliziaji ikiwa imefikia asilimia 98 na kwamba muda mfupi ujao meli ya Mv.Liemba yenye mkataba wa miezi 24 ya ukarabati mkubwa itapandishwa kwenye cherezo ili kuanza kufanyiwa ukarabati huo.

Mwisho.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI