MAMLAKA ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA) kupitia kwa Maafisa wake, Afisa Uhifadhi Mkuu- Masoko, Michael Makombe pamoja na Afisa Uhifadhi Mwandamizi- Uhusiano wa Umma, Kassim Nyaki wameshiriki kipindi mubashara kupitia TBC Safari Channel na Bongo FM kuelezea upekee wa vivutio vya utalii vilivyoko katika hifadhi hiyo ya Ngorongoro.
Maafisa hao wameweza kubainisha shughuli za kihifadhi, gharama za kuingia kutalii Ngorongoro, shughuli ambazo wageni wanaweza kuzifanya wakiwa ndani ya hifadhi na kuelezea namna NCAA inavyoshirikiana na wadau mbalimbali katika kuhusianisha utalii na michezo (Sport Tourism).
0 Comments