Na Gabriel Kilamlya, Matukio DaimaAPP NJOMBE
MKUU wa Mkoa wa Njombe Antony Mtaka, amezitaka taasisi za SIDO, TBS na nyingine zinazohusika kuwasaidia wajasiriamali zifanye kazi ya kuwajengea uwezo wa namna ya matumizi ya Teknolojia katika bidhaa na mazao wanayozalisha ili waweze kuzalisha kwa tija.
Mtaka ametoa agizo hilo katika mkutano wa kuwajengea uwezo wanawake kupitia Chemba ya Wanawake wafanyabiashara Tanzania TWCC mkoani Njombe na kwamba kinachohitajika kwa wanawake wa Njombe ni kuwaonesha Teknolojia za kisasa zinazoweza kuwasaidia.
Aidha Mtaka amesema mkoa wa Njombe una wanawake Matajiri ambao hawahitaji kuendelea kupewa elimu za kujikwamua kiuchumi badala yake waelezwe fursa zinazoweza kuwasaidia.
Rais wa TWCC Tanzania Mercy Silla anasema wamefika Mkoani Njombe kuwasaidia wanawake kuona namna ya kulitumia soko huru la Afrika kupitia uzalishaji wanaoufanya kwani serikali imeingia makubaliano ya Kimataifa katika kunufaika na soko hilo.
Thomas Andrew Mcharo ni Ofisa Biashara toka wizara ya Viwanda na Biashara ambaye anawataka watanzania kutumia Fursa ya soko la Afrika kupeleka bidhaa zao kwani itasaidia kukuza uchumi kwa uwanda mpana.
Kwa upande wao baadhi ya Wanawake mkoani Njombe Akiwemo mwenyekiti wa TWCC Mkoa Marieth Putika wamekiri kuwa mafunzo hayo yatakwenda kuwainua katika Shughuli zao kwani wameoneshwa fursa ya kulitumia soko huru la Afrika.
Mwisho.
Baadhi ya wanawake wa TWCC mkoa wa Njombe.
Rais wa TWCC Taifa Mercy Silla.
0 Comments