Na Hamida Ramadhan Matukio Daima app Dodoma
SHEIKHE wa Mkoa wa Dodoma, Mustapha Rajabu, amewataka Waislamu na wote wanaofuturisha katika mwezi wa Ramadhan kuiga mfano wa Rais Samia Suluhu Hassan, ambaye hivi karibuni aliwaalika wenye uhitaji kufuturu naye Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Akizungumza Leo Machi 7 2025 katika ibada ya swala ya Ijumaa kwenye msikiti wa Gaddafi, Sheikhe Rajabu amesema ni jambo la kushangaza kuona taasisi, kampuni, wizara, na wafanyabiashara wakubwa wakifuturisha watu wasiokuwa na mahitaji.
“Leo hii futari zetu tunawaalika watu ambao hawana haja nazo na hizo yani imekuwa kama fasheni halafu tunajigamba kabisa yakwamba tumefuturusha tunakosea sana ndugu Waislamu " Amesema
Na kuongeza "Hatuwezi kuendelea hivi; kuna watu wenye uhitaji mkubwa, kama wajane na familia zenye shida, ambao wanahitaji msaada,” amesisitiza.
Amempongeza Rais Samia kwa mfano mzuri alioweka na kusema ni muhimu kutambua na kuwasaidia wenye mahitaji katika jamii.
Pia, Sheikhe Rajabu amesisitiza kuwa mwezi wa Ramadhan ni muda wa Kivu na thawabu kutubu, kusameheana, na kuimarisha undugu .
Amesema kuwa Ramadhan ni fursa ya kutenda mema, kutoa sadaka, na kupata thawabu kubwa .
“Huu ni mwezi wa kujiimarisha kimwili na kiroho hivyo niwatake Waislamu wote nchini kuhakikisha hawapitwi na fursa hii kuimarisha mwili na roho” amesema.
0 Comments