Header Ads Widget

WANAWAKE NJOMBE WATAKIWA KUACHA KUWAKATILI WATOTO NA WAUME ZAO.

 



Na Gabriel Kilamlya Matukio DaimaAPP NJOMBE


WANAWAKE Mkoani Njombe wametakiwa kuacha vitendo vya ukatili kwa watoto na waume zao vinavyotajwa kukwamisha jitihada za kukabiliana na ukatili wa kijinsia katika Jamii.


Katika Maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani katika Halmashauri ya mji wa Njombe yaliyofanyika katika kata ya Kifanya Madiwani wa viti Maalumu Tarafa ya Njombe Mjini Tumain Mtewa na Anjela Mwangeni wamesema Wanawake wanatakiwa kuacha ukatili huo ambao umekuwa ukisababisha chuki baina yao,watoto na hata wanaume.


Katibu wa Umoja wa wanawake wa CCM UWT wilaya ya Njombe Zubeda Bilal amewataka wanawake kuwajali watoto ambao wakati mwingine wanajikuta kama Yatima ili Hali Wana wazazi huku Mwenyekiti wa UWT wilaya ya Njombe Beatrice Malekela akiwataka wanawake kupunguza Maneno kwa waume zao.


Kwa niaba ya mkurugenzi wa Halmashauri ya mji wa Njombe,Mganga mkuu wa Halmashauri hiyo Dokta Jabil Juma amewataka Wanawake kujituma kuzalisha pindi wanapowezeshwa ili wasiendelee kuwa tegemezi kwa wanaume.


Enembora Lema ni mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii Halmashauri ya mji wa Njombe ambaye amesema Serikali itaendelea kuwawezesha wanawake kwa kuwapa mikopo isiyo na Riba ili wakuze kipato katika familia.


Akizungumza kwa niaba ya Mgeni wa Heshima katika Maadhimisho hayo Erasto Mpete Mwenyekiti wa Halmashauri ya mji wa Njombe,Diwani wa kata ya Yakobi Michael Uhahula anasema wakati wanawake Wakiadhimisha siku yao wanapaswa kutambua wanaowajibu wa kujikomboa kifikra ili kuondokana na utegemezi.


Tamati ya Maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani Ni Machi nane ambapo Kitaifa yanatarajia Kufanyika mkoani Arusha na kuhudhuriwa na Rais Samia Suluhu Hassan huku katika mkoa wa Njombe yakifanyika huko Bulongwa Makete.


Mwisho.








Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI