Na Hamida Ramadhan, Matukio Daima App Dodoma
BARAZA la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) limefanya tafiti na kuaandaa maandiko ya miradi ambapo Baraza limeratibu utekelezaji wa miradi ya mabadiliko ya tabia nchi, kupunguza matumizi ya zebaki kwa wachimbaji wadogo wa dhahabu pamoja na mradi wa kusimamia utekelezaji wa Sheria ya mazingira.
Hayo yameelezwa leo March 24,2025 Jijini Dodoma na Mkurugenzi Mkuu wa NEMC Dkt. Immaculate Sware Semester wakati akizungumza na waandishi wa habari juu ya mafanikio ya miaka minne ya serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Dkt, Samia Suluhu Hassan
Amesema ajenda ya tafiti imetekelezwa katika maeneo mbalimbali ikiwa ni pamoja utafiti kuhusiana na changamoto za uchafuzi wa Mto Mara; Mmomonyoko wa fukwe za maeneo ya Coco Beach, Kunduchi Beach, Mbweni JKT Beach Club na KJ742 Navy, Fukwe za Mikadi; eneo la Msuka lililopo Pemba Kaskazini; Ghuba ya Mikindani na Manispaa ya Mtwara.
"Baraza limefanya tathmini ya hali ya mazingira kwenye maeneo yanayokumbwa na maporomoko ya ardhi katika milima ya Hanang, Manyara na Mamba Myamba iliyopo Wilayani Same – Kilimanjaro," Amesema..
Na kuongeza "Baraza limefanya tathimini ya Ubora wa Maji ya Ziwa Victoria na kuaianisha maeneo yanayotakiwa kupewa kipaumbele katika suala zima la kulinda ubora wa maji kutokana na athari zilizobainika Ziwa Victoria, " Amesema
Ameeleza kuwa ,Tafiti hizo zimepelekea kuwepo kwa Taarifa mbili za
Development of Environmental Management Strategy Towards Sustaining Ecological integrity of Lake Victoria;Lake Victoria: Roadmap for Management of Water Quality in Mwanza City, Tanzania.
Aidha, Baraza linaendelea na Utafiti Kuhusu Uwezo wa Kuoza kwa Mifuko Mbadala ya Non-Woven. Utafiti huu unafanyika kuainisha ubora na viwango vinavyotakiwa kuzingatiwa katika utengenezaji wa mifuko mbadala isiyo ya plastiki (physical and chemical properties of Non-woven bags) ili kujua uwezekano wa mifuko hiyo kuwa na uwezo wa kuoza (biodegradability).
Vilevile, Baraza limefanya tathmini mbalimbali na kuandaa ripoti zenye ushauri wa jinsi ya kutatua changamoto mazingira kwenye maeneo mbalimbali kama vile mafuriko kwenye maeneo ya Rufiji, na Mkoani Singida na Wilaya ya Mpwapwa Mkoani Dodoma.
Eneo lingine liliofanyiwa tathimini ni pamoja na kwenye maporomoko ya udongo kwenye maeneo ya Milima ya Miamba Myamba (Same), Mlima Kawetere na Mlima Livingstsone (Mbeya), na Mlima Hanang (Manyara); Changamoto za mazingira kwenye Bandari Bubu.
"Eneo lingine ni Tathmini ya hali ya mazingira kwenye maeneo oevu kama vile Kilombero na Malagarasi Moyovosi,".
Amesema katika utekelezaji wa Miradi ya Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabia Nchi, kupitia ithibati (accreditation) ya kuwa msimamizi (National Implementing Entity) wa fedha za Mfuko wa Dunia wa Mabadiliko ya Tabianchi (Adaptation Fund) nchini, Baraza limeweza kuratibu maandako na utekelezaji wa miradi minne kwenye maeneo mbalimbali.
Amesema mradi wa kuhimili mabadiliko ya tabianchi Wilayani Bunda (Mkoani Mara) mradi wa Kuhimili mabadiliko ya tabianchi katika jamii za wakulima na wafugaji wilayani Kongwa (Mkoa wa Dodoma) Mardi wa kuainisha na kutumia teknolojia za kimkakati za uvunaji maji kwa ajili ya kuhimili mabadiliko ya tabianchi katika maeneo kame ya Tanzania (Mikoa ya Dodoma, Singida na Tabora) pamoja na Mradi wa kuhimili mabadiliko ya tabianchi katika jamii za pwani za Zanzibar.
Aidha amesema Baraza limefanya kaguzi katika maeneo 178 ya uzalishaji na usambazaji wa mifuko ya plastiki, ambapo maeneo 57 yalikutwa na makosa na kuchukuliwa hatua stahiki za kisheria.
Hata hivyo amesema zaidi ya Tani 150 za vifungashio visivyokidhi viwango vilikamatwa, vikataifishwa na kuteketezwa kwa mujibu wa Sheria.
"Suala la udhibi wa vifungashio vya plastiki ni letu sote kuanzia ngazi ya familia hadi Taifa hivyo hatuna budi kushirikiana kwa ajili ya kuleta matokeo chanya, " Amesema
Hata hivyo amesema Kwa upande wa Kaguzi na Ufuatiliaji wa Uchafuzi wa Mazingira kwa kipindi cha miaka minne (4), jumla ya kaguzi 9,606 zilifanyika na malalamiko 1,483 yalishughulikiwa hasa katika eneo la kelele na mitetemo.
Amebinisha kuwa ,uchafuzi wa mazingira ulidhibitiwa katika miradi mikubwa yenye viashiria hatarishi (Bwawa la Mwalimu Nyerere, Bomba la Mafuta ( EACOP), SGR n.k), ambapo programu 50 za elimu na vipindi 75 vya uhamasishaji vilifanyika.
Mwisho
0 Comments