Header Ads Widget

CPA VICTOR MAKUNDI ATAKA TLS, TUME YA MAADILI YA MAWAKILI NA MAHAKAMA KUU KUMCHUKULIA HATUA TUNDU LISSU.

 


NA WILLIUM PAUL, HAI.


MJUMBE wa Baraza Kuu la Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi Taifa kupitia mkoa wa Kilimanjaro, Victor Makundi amekitaka Chama cha Wanasheria nchini, Tume ya maadili ya Mawakili na Mahakama kuu kutomfumbua macho mwanachama wao Tundu Lissu anayejaribu kuipoka Katiba ya nchi madaraka yake na kuipaka matope na kumchukulia hatua.


Makundi ametoa kauli hiyo jana, alipokuwa akizungumza na vijana 720 wa Chama cha Mapinduzi waliopo kambini wilayani Hai mkoani Kilimajaro ambapo alisema kuwa, haiwezekani mtu mmoja au kikundi cha watu kikatupoka haki ya kupiga kura nakwani ni haki ya kila Mtanzania kupiga kura na kuwa na uchaguzi.



"Sisi ni vijana wa nchi hii tukishindwa uisimamia Katiba yetu tukiwa wadogo tunaandaa Taifa gani la kesho ni lazima tusimame imara kuhakikisha katiba yetu inalindwa na haipaswi mtu huyu akaendelea kuachwa akilipotosha Watanzania" alisema Makundi.


Alisema kuwa, wapo watu wanaozani kuwa Taifa hili ni la kwao na wanataka kuwavuruga Watanzania kwa maslahi yao binafsi hili halitawezekana na wao kama vijana wa CCM wataendelea kulipigania Taifa.



Mjumbe huyo wa Baraza alisema kuwa, vijana wanaowajibu wa kuitetea na kuilinda Katiba dhidi ya vitisho vya watu wachache wanaotaka kuihujumu kwa maslahi yao binafsi.


Alisema kuwa, kitendo cha Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Lissu cha kudai watahakikisha uchaguzi haufanyiki kauli hii haikubaliki na kutaka kutambua kuwa swala la Uchaguzi katika nchi hii sio swala la familia na si swala la chama kimoja ni matakwa ya Katiba.

 


"Katiba ya Tanzania ya mwaka 1977 na marekebisho yake Ibara ya 65 inasema wazi lazima uchaguzi ufanyike kila baada ya miaka mitano kwa hiyo swala la uchaguzi sio la kujadili wala kubishana hili ni takwa la katiba lazima lifanyike" alisema Makundi.


Na kuongeza "Cha kushangaza kabisa Lissu ni Wakili msomi aliyekula kiapo cha kuilinda na kuisimamia na kuitetea Katiba ya Tanzania na kanuni sasa yeye kama Wakili anaongoza watu kutaka kuivunja Katiba na kuiharibu na kuipaka matope huu ni usaliti kwa taaluma yake na ni usaliti kwa Watanzania".


Aliongeza kuwa, ni ukweli usio na kificho Chadema hawajajipanga kwa ajili ya uchaguzi hivyo wanatafuta visingizio vya kisiasa ili kuhalalisha kushindw kwao .


Chama cha Mapindizu kimeanza kujiandaa muda mrefu kuelekea uchaguzi Mkuu ambapo kimefanya marekebisho ya katiba ya Chama na kuweka mikakati hivyo amewataka kutambua wagombea wa CCM watashinda kwa kishindo.


Mwisho..

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI