Na Shomari Binda-Musoma
Chama cha Mapinduzi ( CCM) Wilaya ya Musoma Vijijini kimemuahidi kumpa ushirikiano wote Katibu mpya wa chama hicho mkoa wa Mara aliyewasili hivi karibuni.
Ikiwa ni ziara yake ya kwanza tangu kuwasiliusoma Vijijini imekuwa ya kwanza kwa Katibu wa mkoa kuitembelea huku akipokelewa na viongozi mbalimbali akiwemo mbunge wa jimbo la Musoma Vijijini Profesa Sospeter Muhongo.
Akizungumza kwenye kikao cha Halmashauri Kuu ya Wilaya mara baada ya mapokezi hayo Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Musoma Denis Ekwabi maarufu kama(Ruto) amemuhakikishia Katibu huyo kumpa ushirikiano wote kama chama.
Amesema chama Wilaya ya Musoma vijijini kipo salama na wanafanya kazi kwa ushirikiano kuanzia ngazi za mashina,mkoa hadi taifa.
Ekwabi amemueleza Katibu huyo baada ya kufanya vizuri kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa wanajipanga vizuri kwenye uchaguzi mkuu mwezi oktoba kwa kushinda kwa kishindo kuanzia nafasi za udiwani,ubunge hadi urais.
" Tunakukaribisha sana Kstibu Wilaya ya Musoma Vijijini kichama na tunakuahidi kukupa ushirikiano wote kwenye shughuli za chama.
" Chama kipo salama na tunafanya kazi kwa ushirikiano viongozi wote kuanzia ngazi ya mashina kuhakikisha malengo yanatimia ikiwa ni pamoja na kushika dola",amesema.
Mwenyekiti huyo amesema chama kinampa ushirikiano mbunge wa jimbo Profesa Sospeter Muhongo na anatekeleza vizuri ilani ya uchaguzi kwa kuwa miradi mingi inatekelezwa jimboni na kuwaletea wananchi maendeleo.
Ekwabi amesema Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan amefanya kazi kubwa katika utekelezaji wa ilani kwa kipindi cha miaka 4 hivyo malipo kwake ni kumtafutia kura na kushinda kwa kishindo kwenye uchaguzi mkuu 2025.
Katibu wa Chama cha Mapinduzi ( CCM) mkoa wa Mara Iddy Mkoa amesema mkoa wa Mara na ataanzia walipoishia watangulizi wake akiwemo aliyemuachia ofisi Ibrahim Mjanakher.
Amesema moja ya muendelezo huo ni kuwaunganisha wanachama wa CCM kuendelea kuwa kitu kimoja na kushirikiana katika majukumu ya kazi.
Iddy amesema pasipo kuwa na umoja na kufanya kazi kwa kushirikiana kuanzia kwa viongozi wa ngazi zote za chama na jumuiya zake mambo hayawezi kwenda.
Amesema amekuja mkoa wa Mara kuendeleza pale walipoishia watangulizi wake na kuomba ushirikiano wa kila moja ili kila lililokusudiwa na chama liweze kufanikiwa.
Katibu huyo amesema mwaka huu ukiwa mwaka wa uchaguzi unahitajika umoja na ushirikiano zaidi ili kuweza kufanya vizuri kwenye uchaguzi huo kuanzia nafasi ya udiwani,ubunge hadi uraisi.
" Nishukuru nimepata mapokezi mazuri na viongozi wenzangu wa ngazi ya mkoa back hapa Musoma Vijijini nilipofika leo.
" Kadri ya muda ntakutana na viongozi mbalimbali pamoja na wanachama kule kwenye matawi lakini kubwa nimekuja kuendeleza pale walipoishia wenzangu",amesema.
Mwisho.
0 Comments