Header Ads Widget

MIGOGORO YA ARDHI, MADAI YATIKISA ARUSHA.


Mkurugenzi wa huduma za msaada wa kisheria Esther Msambazi kutoka wizara ya katiba na sheria  akiongea na waandishi wa habari mkoani Arusha.


.Wanaume wajitokeza kwa Wingi.

.Migogoro 136 yapatiwa Ufumbuzi papo hapo.YAPATA 


NA NAMNYAK KIVUYO, ARUSHA.


KUFUATIA kuwepo kwa Msaada wa kisheria unatolewa na Wizara ya Katiba na Sheria kupitia kampeni ya Samia Legal Aid inayoendelea mkoani Arusha, kuelekea maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani  migogoro ya Ardhi na madai imeonekana kuwepo kwa asilimia kubwa huku 136 ikipata ufumbuzi katika maonyesho hayo.


Akiongea na waandishi wa habari katika utekelezaji wa kampeni hiyo mkurugenzi wa huduma za msaada wa kisheria Esther Msambazi kutoka wizara ya katiba na sheria amesema kuwa wameweza kuwafikia wananchi 1844  huku wengi wao wakiwa ni wanaume .


Msambazi amesema kuwa migogoro iliyoongoza ni migogoro ya ardhi ikifuatiwa na migogoro ya madai tofauti na mikoa mingine ambapo mingi baada ya ardhi inafuatiwa na  masuala ya ukatili wa kijinsia na mirathi lakini kwa  Arusha wameona migogoro mingi ya madai.



"Kwa hizi siku saba tulizokuwa hapa tumeweza kuwafikia wananchi 1844 na tumepokea migogoro 677 na kati yake tumefanikiwa kutatua migogoro 136 kwa kuwapatanisha na kutatua changangamoto zilizokuwa zikiwakabili," Amesema Msambazi



"Migogoro mingi imewasilishwa na wanaume, inawezekana wanaume wana changamoto zaidi kuliko wanawake lakini pia inawezekana wamezineba changamoto hizo kama baba wa familia ndio maana tumeona wengi wamejitokeza kuziwasilisha,"Ameeleza


Ameeleza kuwa  asilimia kubwa wamefanikiwa kuitatua kwa pande zote mbili kuweza kukaa na kukubaliana na lile lengo ambalo kama serikali walipanga kulifikia limefanikiwa kwa sehemu kubwa na mingine inaendelea, kwani kuna zilizopo mahakamani lakinj  mingine wanashughulikia kiutawala na itaendelea kufuatiliwa na yote itahitimishwa kwa jinsi ilivyo wasilishwa.


Amefafanunuwa kuwa wamewapa elimu, msaada wa kisheria lakini pia kutatua migogoro ambapo wamemetumia nafsi hiyo  kuwaandikia makubaliano, kuwawasilisha mahakamani wale ambao migogoro yao ilikuwa ina uhutaji wa kwenda mahakamani kwasababu kampeni imewajumuisha wadau kutoka maeneo mbalimbali wakiwemo mawakili wa kujitegemea.


Ameendelea kusema kuwa lengo la kampeni hiyo ni kuhakikisha wanawa elimisha wananchi katika ngazi za kijamii kuhusiana na masuala mbalimbali ya kisheria na namna gani wanaweza kuifikia haki na kutatua migogoro ambapo hadi kufikia february 25,2005 wameshatekeleza kampeni hiyo mikoa 22.


Mwisho.








Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI