Header Ads Widget

MBUNGE KIBAMBA AKUMBUSHA WANANCHI KUJIANDIKISHA KWENYE DAFTARI LA WAPIGA KURA

 

Na MWANDISHI WETU, MATUKIO DAIMA App

MBUNGE wa Kibamba, wilayani Ubungo, Dar es Salaam, Issa Mtemvu (CCM) amewakumbusha wananchi kujitokeza kujiandisha na kuboresha taarifa zao kwenye uandikishaji Daftari la wapiga kura (DKW).


Mtemvu aliyasema hayo jana Machi 17, 2025 akiwa kwenye Kituo cha Kibwegere Shule, Mtaa wa Kibwegere Kata ya Kibamba mkoani Dar es Salaam alipokwenda kuboresha taarifa zake kwenye daftari hilo.


Alisema huu ni muda wa wananchi wa Kibamba kujitokeza kwa wingi kujiandikisha na kuboresha taarifa zao kwenye Daftari la kudumu la Mpiga kura ili  ili baadaye waweze kupata fursa ya kuchagua viongozi kwenye uchaguzi mkuu baadaye mwaka huu.


"Hili linakwenda sambamba  na kuandikisha wapigakura wapya lakini linalenga kuboresha pia taarifa za wapiga kura wa zamani wakiwemo wale waliopoteza kadi zao. Hivyo wananchi hawana budi kujitokeza na kutumia nafasi hii kukamilisha zoezi hili la uandikishaji na uboreshaji wa taarifa zao" alisema Mbunge huyo. 


Kwa mujibu wa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila,  uandikishwaji huo utafanyika kwa siku saba na umeanza jana Machi 17 na utakamilika 23 Machi, 2025.

Chalamila alisema uandikishwaji huo unawahusu wale waliotimiza miaka 18, waliopoteza kadi zao, na wale ambao kadi zao ziliharibika watapatiwa nyingine.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI