Header Ads Widget

DKT BASHIR TWEVE:UKOMO WA WABUNGE WA VITI MAALUMU KULETA WANAWAKE MASHUPAVU KAMA MAMA SAMIA

 


NA MATUKIO DAIMA MEDIA 

Mjumbe wa Halmashauri kuu Chama Cha Mapinduzi (CCM)  Wilaya Mufindi kupitia Jumuiya ya wazazi Dkt.Bashir Tweve amesema kuwa Chama kimefanya uamuzi mzuri wa kuweka ukomo wa wabunge wa viti maalumu kwasababu kupitia hili chama kinakwenda kupata wanawake mashupavu kama Dkt Samia Suluhu Hassan.

Tweve ameeleza hayo alipokuwa akielezea uamuzi uliofanywa na Chama cha Mapinduzi (CCM) juu ya ukomo wa nafasi ya ubunge, uwakilishi na udiwani wa viti maalumu uliotangazwa na CCM kupitia kikao maalum cha Halmashauri Kuu ya CCM Taifa siku ya March 10, 2025 kilichojadili ajenda mbalimbali ikiwemo ukomo wa wabunge.

“Kwanza niipongeze Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM) kupitia Mwenyekiti wetu Dkt Samia Suluhu Hassan kwa maamuzi mahususi ambayo  yamefanywa ya ukomo wa wabunge wa viti maalumu  kwasababu kupitia hilo tunakwenda kupata wanawake mashupavu ambao wanauzoefu wa kutosha na wanaojua  bunge ni nini na majukumu yao ni yapi na hili ni kupitia nafasi mbalimbali za uongozi ambazo wamekuwa wakizitumikia na mfano halisi tunaye Rais wetu Dkt. Samia Suluhu Hassan ambaye kwa kipindi flani alikuwa Mbunge lakini sasa ni Rais kwaio kuna makuzi flani ndani ya ubunge ambayo kupitia ukomo yanaibua ushupavu”

Hata hivyo Tweve amewataka viongozi kupitia jumuiya ya wazazi katika ngazi ya wilaya, kata na matawi kuweza kutenga muda katika kuhakikisha kuwa wanatoa elimu  kwa wazazi na walezi wa watoto wenye ulemavu na wenye  changamoto mbalimbali ili kuona umuhimu wa kuwapeleka Watoto wao kwenye taasisi na vituo vya kujifunzia na sio kuwaficha ndani.

“Mimi naomba nitoe rai kupitia jumuiya ya wazazi kwamaana ngazi ya wilaya, kata na matawi tuende tusaidiana kuwaelimisha wazazi na walezi wa watoto wenye ulemavu  na changamoto mbalimbali wawaibue wawalete kwa wadau na Taasisi husika ili waweze kuwasaidia na hii itakuwa rahisi kama tukishawajua wazazi ili kuweza kuwaunganisha na Taasisi mbalimbali”

Pia ametoa pongeza kwa Taasisi ya Foxes Community and Wild life Conservation na Mradi wa Youth Agency Mufindi (YAM)  kwa kuweza kuona uhitaji wa vijana wenye ulemavu na kuwapatia mafunzo ya ujasiriamali huku akieleze umuhimu wa mafunzo hayo kwa jamii na vijana wenye changamoto.

“kama Mjumbe wa Halmashauri kuu kupitia Jumuiya ya wazazi  ambapo pia tuna  kitengo cha malezi Kwa vijana na watoto  nitoe pongezi kwa Taasisi ya Foxes Community and Wild Life Conservation na Mradi wa Youth Agency Mufindi (YAM) ambao wamejitoa kusaidia vijana wenye changamoto ya ulemavu na  uzuri ni kwamba hao wanaposaidika wanawapa hamasa na wale wengine ambao wapo nyumbani na hata wale waliowaficha watoto kushawishika kuwaleta Watoto hao katika Taasisi husika”

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI