KATIKA kuadhimisha miaka 30 ya Mamlaka ya Elimu na mafunzo ya Ufundi stadi VETA sambamba na miaka Hamsini ya mfumo wa kitaasisi wa elimu na mafunzo ya Ufundi stadi nchini Tanzania, chuo cha ualimu wa ufundi stadi Morogoro wameweka wazi azma yao ya kuongeza kiwango cha usahili wa wanafunzi Walimu kutoka 500 wa mwaka huu kufikia wanafunzi 3100 ifikapo mwakani ili kwenda sambamba na mahitaji ya walimu amali nchini.
Mkakati huo wa MVTTC unalenga kukabiliana na mahitaji ya sasa ya maboresho ya mtaala ya kufundishia na kujifunzia kwa shule za msingi na sekondari ambapo wanafunzi sasa wanajifunza mkondo wa Amali yanayolenga zaidi kuwapa wanafunzi ujuzi kwenye stadi mbalimbali za ufundi ambapo suala la Walimu kwaajili ya kufundishia litakuwa ni kipaumbele kwa shule.
Mkuu wa chuo cha ualimu wa ufundi stadi Morogoro Samwel Kaali Alisema hayo wakati wa maadhimisho hayo mjini Morogoro yaliyokwenda sambamba na kuanza kwa ukarabati wabkarakana ya fani ufundi wa chuma na uchomeleaji katika karakana ya shule kongwe ya Ufundi ya Msamvu ambayo ina wanafunzi wa kawaida na wale wenye mahitaji maalum.
Akasema baada ya upanuzi wa miundo mbinu ya chuo hicho cha ualimu wa ufundi ikiwemo mabweni na karakana wameongeza mtaala mipya 18 ili kwenda sambamba na mahitaji ya Soko.
Kaali akasema wameguswa kukarabati karakana hiyo sambamba na kurekebisha mfumo wa Umeme baada ya kubaini mahitaji makubwa ambayo shule hiyo kongwe yenye wanafunzi 155 inakabiliwa nayo.
Akasema maadhimisho hayo yanalenga kutambua mchango wa elimu na mafunzo ya ualimu wa ufundi Katika kuendeleza elimu na mafunzo ya Ufundi stadi nchini.
Akasema wameamua kushiriki maadhimisho hayo kwa kukarabati karakana hiyo kama sehemu ya shughuli za kujitolea Katika kusaidia kuboresha huduma za jamii.
"ukarabati huu unaofanyika Katika karakana hii ya fani ya chuma na uchomeleaji utahusisha kuboresha mfumo wa umeme, kuezua paa la zamani na kuweka jipya, pamoja na kuweka sakafu ya zege"Alisema Mkuu huyo wa MVTTC .
Akasema pia wamekabidhi vifaa na nyenzo za kujifunzia na kufundishia masomo ya Ufundi kwa Uongozi wa shule hiyo ili nisaidie masomo ya Ufundi stadi.
Kwa upande wake Mwalimu Mkuu wa shule ya Ufundi Msamvu Bi Lydia Molel licha ya kushukuru kwa msaada huo akasema umekuja kuwavisha nguo kwani mahitaji waliyo nayo kwenye miundo mbinu na vifaa bado ni makubwa sana.
Aidha akasema masomo ya Ufundi uashi yamewasaidia kupata kipato cha kuboresha baadhi ya Majengo ambayo ni chakavu hususani eneo ambalo sasa wanatumia kama ofisi ingawa bado Wana changamoto nyingi ikiwemo mahitaji ya vyoo na uchakavu wa Majengo mengine na uhaba wa karakana, jiko na Majengo mengine.
Nao baadhi ya wanafunzi waliosoma Katika shule hiyo mwaka 2022 akiwemo Husein Msagati walisema licha ya masomo waliyopata shuleni hapo kuwaonesha njia ya maisha hata kama bado hawajafanikiwa Sana,bado shule waliyowahi kusoma ina changamoto nyingi zinazohitaji kutatuliwa.
Msagati akasema Choo kilichopo wanalazimika kukifuata mbali na wanachangia na wanafunzi wa shule ya Msingi huku karakana moja iliyopo wakitumia kwa zamu kwa kusubiriana kwasababu haitoshelezi kwa fani zote za ufundi.
Kaimu Afisa Elimu ya Msingi Manispaa ya Morogoro, Amina Kova, Alisema shule hiyo inayotoa elimu Katika fani za chuma na uchomeleaji, sayansi kimu ikiwemo ushonaji na mapishi, Uashi na Umeme wa majumbani imekuwa na msaada mkubwa kwa vijana waliokosa elimu Katika mfumo Rasmi ambao kama wasingesaidika wangekuwa wamejiingiza kwenye vitendo viovu mtaani
Akasema ujuzi wanaoupata wanafunzi hao watautumia kupata kipato kwani sekta ya Ufundi kwa sasa ina Ajira za kutosha zinazoonekana ikiwemo Ujenzi wa nyumba mpya, ununuzi wa magari, sherehe zinazohitaji vyakula na mapambo, nguo zinashonwa hasa na kina mama kila siku nk.
MVTTC, Odiface Tarimo akizungumzia Sana zilizokabidhiwa Alisema zimebuniwa na wanafunzi wenyewe lengo likiwa kutengeneza uhalisia wa Kile wanafunzi watakachokwenda kufanyia kazi na kwamba Sana hizo zinaondoa changamoto ya gharama kubwa kununua vifaa halisia kwaajili ya kufundishia.
0 Comments