Header Ads Widget

MAUZO YA MADINI NJE YA NCHI YAONGEZEKA


NAIBU Katibu Mkuu Wizara ya Madini Msafiri Mbibo amesema kuwa, thamani ya mauzo ya madini nje ya nchi pia imeongezeka kwa kasi,ikifikia dola za Marekani milioni 3,551.4 mwaka 2023, kutoka dola milioni 3,395.3 mwaka 2022.

Ongezeko hilo la asilimia 4.6 linaonesha jinsi sekta hii inavyoendelea kuwa tegemeo la mapato ya kigeni kwa Tanzania. Kwa sasa, madini yanachangia asilimia 56.2 ya mauzo yote ya bidhaa zisizo za asili nje ya nchi, jambo linaloifanya sekta hii kuwa mojawapo ya sekta zenye mchango mkubwa katika uchumi wa Taifa.

Aidha Mbibo ameongeza kuwa, mbali na ongezeko la mapato na uwekezaji, Wizara ya Madini imefanikiwa kutekeleza miradi mingine muhimu, ikiwa ni pamoja na:

Ununuzi wa mitambo 10 ya uchorongaji (rigs) kwa ajili ya kuwezesha wachimbaji wadogo kupata madini kwa urahisi na kwa teknolojia ya kisasa.



Utoaji wa leseni kubwa ya uchimbaji wa madini ya kinywe (SML) kwa Kampuni ya EcoGraf Limited, inayofanya kazi katika eneo la Epanko, Wilaya ya Mahenge – Morogoro.

Pamoja na kukamilika kwa utafiti maalumu na kuchora ramani ya jiolojia ya visiwa vya Zanzibar (Unguja na Pemba) ili kubaini fursa zaidi za madini katika eneo hilo.







Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI