Watoto yatima wanaolelewa kwenye kituo cha Manara Ujiji mkoani Kigoma wakipata Futari ya mwezi mtukufu wa Ramadhani iliyoandaliwa na Makamu wa Rais Dk.Philip Mpango
Na Fadhili Abdallah,Habari na Matukio App Kigoma
MAKAMU wa Raisi Dk.Philip Mpango ametoa futari kwa wanawake wajane na kufuturisha Watoto yatima zaidi ya 300 katika manispaa ya Kigoma Ujiji mkoani Kigoma.
Futari hiyo imekabidhiwa kwa wajane hao kwa niaba ya Makamu wa Raisi na Shekhe wa mkoa Kigoma,Hassan Kiburwa ambapo Shekhe Kiburwa alisema kuwa Makmu wa Raisi amekabidhi futari hiyo ikiwa kutimiza matakwa ya dini ya kuwasaidia wenye uhitaji katika mwezi huu mtukufu wa Ramadhani.
Shekhe wa mkoa Kigoma Hassan Kiburwa (kulia) akikabidhi futari kwa wanawake wajane wa manispaa ya Kigoma Ujiji iliyotolewa na Makamu wa Rais Dk.Philip MpangoShekhe Kiburwa alisema kuwa imekuwa kawaida ya Makamu wa Raisi kuwasaidia wenye uhitaji mkoani humo ikiwemo waumini wa kiislam na kwamba anafanya hivyo kwa mapenzi na ubinadamu wake bila kujali itikadi za dini.
Sambamban a kutoa futari kwa wajane hao ambao walikabidhiwa mchele, sukari,unga wa ngano na maharage pia Jumapili jioni alitarajia kuwafuturisha Watoto yatima zaidi ya 300 wanaohifadhiwa kwenye kituo cha Manara Ujiji mkoani Kigoma.
Baadhi ya wanawake wajane waliopokea futari hiyo akiwemo Moza Mohamed alimshukuru Makamu wa Raisi kwa msaada huo wa Futari kwa wanawake wajane mkoani Kigoma kwamba anaonyesha kujali hali za watu wa kipato cha chini bila kujali dini zao.
0 Comments