Header Ads Widget

JACCAFO WAPONGEZWA KULETA MABADILIKO YA USAWA WA KIJINSIA SIMIYU

MJUMBE na Mwakilishi wa Taasisi ya JACCAFO, Janeth Epaphra akipokea Cheti Maalum cha Pongezi toka Kwa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Kenani Kihongosi kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa shirika hilo,Joseph Ngeleja kama Taasisi Kinara katika kuleta mabadiliko ya usawa wa kijinsia mkoani Simiyu, kwenye maadhimisho ya siku ya Wanawake kimkoa yaliyofanyika Busega, March 3, 2025.


Na COSTANTINE MATHIAS, Simiyu.


TAASISI ya Taasisi ya Juniors and Child Care Foundation (JACCAFO) yenye Makao Mkuu wilayani Maswa Mkoani Simiyu imepongezwa kwa kuendelea kuleta mabadiliko ya Usawa wa Kijinsia kwenye maadhimisho ya siku ya Wanawake yaliyofanyika March 3, wilayani Busega Mkoani Simiyu.


Akipokea cheti kwa niaba ya Taasisi hiyo, Mjumbe wa JACCAFO Janeth Epaphra, amesema cheti hicho ni ishara ya serikali kutambua shughuli zinazofanywa na Taasisi hiyo binafsi katika kutetea Usawa wa Kijinsia.


 Awali Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Kenani Kihongosi @kenan ameyapongeza mashirika binafsi kuendelea kutambua mchango wa Wanawake katika shughuli za Maendeleo huku akiwasisitiza Wanawake kujitokeza kushiriki Uchaguzi Mkuu utakaofanyika mwishoni mwa mwaka huu.


Mwisho.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI