Header Ads Widget

DEREVA MATATANI KWA TUHUMA ZA KUCHOMA MOTO GARI YA MAFUTA BAADA YA KUFANYA WIZI

 



JESHI la Polisi Mkoani Morogoro limefanikiwa kumtia mbaroni Bwana Abubakar Adam Mwichangwe (29) ambaye ni Dereva na mkazi wa Tabata Kinyerezi jijini Dar-es-salaam aliyekuwa akitafutwa kwa tuhuma za kula njama ya kuiba mafuta aina ya Dizel lita 35,700 kisha kuharibu lori lilikokuwa awali  na mafuta hayo kwa kulichoma moto.

Akizungumzia hujuma hiyo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro SACP Alex Mkama amesema dereva huyo aliyekuwa akiendesha. Lori la mafuta Mali ya kampuni ya Meru Lori lenye namba za usajili T.661 BXW tela namba T.489 BHC aliiba mafuta hayo na kuyashusha kwenye Vituo viwili tofauti vya mafuta vya Simba Oil kilichopo Mkambarani na kingine kilichopo mjini Morogoro.


Aidha alikwenda kulichoma moto Lori hilo katika eneo la Misufini Kijiji cha Msimba barabara kuu ya Morogoro -Iringa Ili ionekane ni ajali..

Tukio hilo kwa mujibu wa polisi lilitokea Machi 16, 2025 na thamani ya mafuta hayo ni Tsh.77,112,000/ mali ya kampuni Acer Logistics (T) yaliyokuwa yakisafirishwa na kampuni ya Meru kwenda Lubumbashi nchini Congo DRC.


Mwisho.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI