Header Ads Widget

POLISI TABORA YAMSHIKIRIA ASKARI ALIYESHIRIKI KUKINGA MAFUTA KWENYE AJALI.

 TAZAMA FULL VIDEO TRAFIKI ALIYEKAMATWA AKIKINGA MAFUTA BOFYA LINK HII


Na Lubango Mleka, Habari Matukio  App - Tabora. 

JESHI la Polisi Mkoa wa Tabora linamshikilia Askari wa Kikosi cha Usalama Barabarani kutoka kituo cha Polisi Wilaya ya Igunga Mkoani Tabora  WP. 8033 PC Victoria kwa kosa la uzembe na kushiriki kukinga mafuta  kwenye gari lililopata ajali katika kijiji cha Igogo Kata ya Igunga. 

Akitoa taarifa kwa Waandishi wa Habari mkoani hapa juu ya tukio hilo la ajali iliyohusisha magari ya mizigo matatu, Kamanda wa Polisi mkoa wa Tabora Richard Abwao amesema Jeshi hilo limemkamata Askari wa Kikosi cha Usalama Barabarani wilaya ya Igunga WP. 8032 PC Victoria kwa kosa la uzembe na kushiriki kumpatia dumu mwananchi kukinga mafuta katika gari lililopata ajali. 


Aidha, Kamanda Abwao amesema ajali hiyo  imesababishwa na uzembe wa dereva wa gari aina ya Scania Tenka lenye namba za usajili T. 275 EK lenye tela namba T. 944 NZ lililokuwa linatoka Dar es Salaam kwenda Nzega kuligonga gari aina ya Scania lenye namba T. 39 DUK lenye tela namba 302 DWD lililokuwa linatokea Kagera kwenda Moshi na lilikuwa limebeba mahindi likiendeshwa na dereva Christopher Msoso, 


Ambalo lilipoteza mwelekeo na kugonga gari jingine lenye namba T. 195 BSC  Scania lenye tela namba T. DRW likitokea Congo kwenda Da es Salaam ambalo lilikuwa halina mzigo. 

" Katika ajali hiyo mtu mmoja aliyefamika kwa jina la Nassoro Ally alijeruhiwa na amelazwa Hospitali ya wilaya ya Igunga kwa matibabu zaidi na tunamshikiria dereva wa gari lililosababisha ajali na kuharibu mali," amesema Kamanda Abwao.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI