Wajumbe wa Bodi ya Wadhamini ya Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) wamekutana leo Machi 10, 2025 Wilayani Tarime, Mkoani Mara kwa ajili ya kuanza kikao cha kawaida cha 209 cha Bodi hiyo kinachoongozwa na Mwenyekiti wa Bodi Jenerali (Mstaafu) George Marwa Waitara.
Kikao hicho cha siku nne kimewakutanisha wajumbe hao ili kujadili masuala mbalimbali yanayohusu Maendeleo ya Shirika ambalo lina dhamana ya kusimamia jumla ya Hifadhi za Taifa 21 nchini.
0 Comments