Header Ads Widget

ALIYEJIFANYA LUTENI FEKI APANDISHWA KIZIMBANI.




Na COSTANTINE MATHIAS, Simiyu.


NCHAMBI Nsungwa Mapanda kwa jina maarufu Emanuel Gangala (24) mkazi wa Mtaa wa Sima katika Halmshauri ya mji wa Bariadi Mkoani Simiyu, aliyejifanya Mwanajeshi wa JWTZ amefikishwa mahakamani kwa makosa matatu.


Awali imedaiwa mahakamni hapo na Mwendesha Mashitaka toka Ofisi ya Taifa Mashitaka, Betrice Mboya mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi wa Mahakama ya Mkoa wa Simiyu Alex Mtenga kuwa mnamo tarehe 14.2.2025 huko katika eneo la shule ya Sekondari Simiyu,  


Inadaiwa kuwa alijitambulisha kuwa yeye ni Afisa wa Jeshi la wananchi mwenye cheo cha Luteni ambapo aliwahadaa watu mbalimbali kuwa angewasaidia kuwaingiza Jeshi la Wananchi na Usalama wa Taifa.


Huku jambo hilo ni kosa chini ya kifungu 100 (b) na kifungu 35 cha sheria ya mwenendo wa makosa jinai sura16 kama ilivyofanyiwa marejeo mwaka 2022.


Katika Shitaka la pili ameshitakiwa kwa kosa la kukutwa amevaa sare zajeshi la wananchi wa Tanzani zenye cheo cha Luteni, ambapo kifuani ilikuwa  kulikuwa na nembo iliyokuwa imeandika Emanuel jambo ambalo ni kinyume cha sheria namba 178 kifungu kidogo1.2.3cha sheria ya mwenendo wa makosa ya jinai.


Na katika shitaka la tatu mshitakiwa ameshitakiwa kwa kosa la kupatikana na sare za jeshi la wananchi ikiwemo mikanda miwili ya jeshi na kofia ya kijeshi yenye rangi ya kijani kinyume cha sheria kifungu namba 312cha sheria ya makosa ya jinai sura16 kama ilivyofanyiwa marejeo mwaka 2022.


Baada ya kusomewa mashitaka yote matatu mshitakiwa amekana makosa yake na kuomba dhamana ambapo hakimu mtenga aliwauliza upande wa mashitaka kama kuna pingamizi lolote kuhusu dhamana ambapo walisema hakuna pingamizi.


Ndipo Hakimu alipomueleza mshitakiwa kuwa dhamana ipo wazi na kwamba mshitakiwa anatakiwa kuwa na wadhamini wawili ambao ni watumishi wa serikali ambao wanatakiwa kuwa na vitambulisho vya Taifa (NIDA) na Barua za watendaji wanakoishi ambapo wanatakiwa kusaini dhamani ya shilingi Mil. tano kwa kila mmoja.


Hata hivyo mshitakiwa alishindwa kutimiza masharti hayo na kurudishwa Lumande na Hakimu Mtenga ameharisha kesi hiyo hadi tarehe 11.3.2025 kesi itakupokuja kwa ajili ya mshitakiwa kusomewa hoja za awali, kutokana na mwendesha mashitaki kuieleza mahakama hiyo kuwa upelelezi wa kesi hiyo umekamilika.


Mwisho.



Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI