Header Ads Widget

WATANGAZAJI ZUNGUMZENI KISWAHILI FASAHA -WAZIRI PROF KABUDI

Na Hamida Ramadhan, Matukio Daima App Dodoma

WAZIRI wa Habari Sanaa Utamaduni na Michezo Profesa Palamagamba Kabudi amevitaka vyombo vya habari kuelimisha jamii namna bora ya kuzungumza, kuandika kiswahili sanifu na kuacha kukifubaza kiswahili. 


Amesema siku za hivi karibuni watanzania wamekuwa wakibananga kiswahili na kuacha kuzungumza kiswahili fasaha. 



Ameyasema hayo Leo jijini Dodoma kwenye Mkutano wa mwaka wa Vyombo vya Utangazaji Nchini unaofanyika siku mbili ambapo amesema kumekuwa na mabadiliko makubwa katika matumizi ya Kiswahili katika vyombo vya habari.


 Amesema hali hiyo inachangia katika mtazamo wa jamii kuhusu lugha na utamaduni. 


Ameeleza utangazaji unapaswa kuwa daraja la kuunganisha watu, kuna tatizo la kupungua kwa matumizi sahihi ya Kiswahili.

"Vyombo vya habari kama redio na televisheni vina jukumu muhimu katika kufundisha na kukuza Kiswahili sanifu Hata hivyo, baadhi ya redio zimejikita zaidi kwenye burudani kama michezo na muziki, badala ya kuzingatia mawasiliano yenye tija, " Amesema 

Na kuongeza "Hii inasababisha mabadiliko katika mtindo wa lugha na hata kushindwa kueleweka kwa baadhi ya vipindi, " Amesema


Aidha ametoa rai kwa vyombo vya habari katika kipindi hiki cha uchaguzi, ni muhimu kutende haki bila upendeleo wa kisiasa. 

"Hii ni njia mojawapo ya kujenga uaminifu katika jamii na kuimarisha demokrasia vilevile, kuna umuhimu wa kuhamasisha matumizi sahihi ya Kiswahili ili kuboresha mawasiliano na kupunguza dhana potofu kuhusu lugha yetu, "Amesema.

Na kuongeza "Kwa hivyo, tunahitaji kuimarisha jitihada za kutangaza vipindi vinavyotumia Kiswahili sanifu na kufundisha umma hii itachangia si tu katika kuleta umoja na amani, bali pia katika kuimarisha utamaduni wetu wa Kiswahili, "amesema.


Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu TCRA Dkt.Jabir Bakari amessma wao jukumu lao kubwa ni kuhakikisha wanasimamia vyombo vyote vya utangazaji na habari Nchini na ni Rai yao kwamba kila chombo kinafuata misingi ya uandishi. 

Aidha ametoa Rai kwa vyombo ambavyo havijasajiliwa kujisajili ili viweze kutambulika na kufanya kazi kwa kufuata misingi na kanuni zinazotakiwa. 

Naye katibu Mkuu wa Wizara hiyo na Msemaji Mkuu wa Serikali Gerson Msigwa ameishukuru TCRA kwa kuweza  kuwa na mikutano kama hii Mara kwa Mara kwani hapo zamani hakukuwa na utaratibu kama huu. 


"Huu utaratibu mliyouweka TCRA ni mzuri kwani hapo zamani waandishi hawakupata semina na mikutano kama hii lakini hivi sasa mmeweka utaratibu mzuri utakaowasaidia kufanya kazi kwa weledi na kusimamia maadili ya uandishi"

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI