Header Ads Widget

TATIZO LA MAJI DAR ES SALAM KUMALIZIKA BAADA YA UJENZI WA BWAWA LA KIDUNDA



Na Lilian Kasenene,Morogoro

Matukio DaimaApp 

UJENZI wa Bwawa la Kidunda lenye uwezo wa kutumza maji lita Bil 190 itasaidia upatikanaji wa huduma za maji katika mikoa ya Pwani na Dar es salaam huku gharama za ujenzi huo zikiwa kiasi cha sh Bil 336.

Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar Es Salaam (DAWASA) Mhandisi Bwire Mkama alieleza hayo katika ziara ya Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) waliotembelea ujenzi wa mradi huo kwa lengo la kujionea hatua iliyofikia ya utekelezaji.

Mkama alisema kuwa Jiji la Dar es salaam limekuwa likikutana na changamoto ya upatikanaji wa maji hususani kipindi cha kiangazi hivyo kukamilika kwa Bwawa la Kidunda litakwenda kumaliza changamoto na kuboresha huduma ya majisafi na salama.

Mradi wa bwawa la Kidunda kwa Sasa imefikia zaidi aslimia 27 za utekelezaji wake ambapo mara baada ya kukamilika litasaidia kuboresha upatikanaji wa huduma ya maji katika Mikoa hiyo.

"Kama ambazo tumewasilisha kwenye taarifa yetu,tangu tumepata uhuru Mwaka 1961 bwawa lilikuwa kwenye makaratasi lakini Serikali ya awamu ya sita imetekeleza kwa gharama za ndani za Serikali,"alisema

Alisema bwawa la Kidunda liko katika mkondo wa mto Ruvu alo ndio chanzo kikubwa cha maji katika maeneo ya mikoa ya Dar es salaam na Pwani ambao ni zaidi ya asilimia 87 ya Maji yote yanayozalishwa katika eneo la Ruvu yanategea Ruvu.

Alisema,kutokana na changamoto ambayo imekuwa ikijitokeza mara kwa mara katika miaka ya nyuma ya kupunguza kwa kina kutokana na hali ya hewa, maji katika mto Ruvu yamekuwa yakileta madhala makubwa kwenye uzalishaji maji na kuathiri upatikanaji wa huduma ya maji kwa matumizi ya bindamu na kiuchumi maeneo hayo.





Meneja Sehemu ya Mazingira na uratibu wa Jumuiya za watumia maji kutoka Bodi ya Maji Bonde la Wami/Ruvu Janeth Kisoma alibainisha kuwa Bwawa la Kidunda ni miongoni mwa vyanzo vya maji vinavyosimamiwa na Wami/Ruvu huku akieleza mipango iliyopo ya kulitangaza kuwa eneo tengefu.

Janeth alisema kuwa Bodi imekuwa ikishirikiana na wadau mbalimbali katika kuhifadhi mazingira ambapo mpaka sasa zaidi ya Mabiriki 29 ya kunyweshea mifugo yameshajenga kwenye vijiji vinavyouzunguka Mto Ruvu ili mifugo is isiweze kuingia mtoni na kuharibu chanzo hicho cha maji.

"Jukumu letu ni kulinga na kuhifadhi  vyanzo vya maji na majukumu haya yanafanyika chini ya usimamizi kwa wa Sheria ya rasilimali za maji namba 11/2009 yenye marekebisho yake namba 8/2022,"alisema.

Bodi ya Maji bonde la Wami Ruvu limekuwa likisimamia vyanzo vya maji 283, ikiwemo mbwawa, visima, mito, chemichemi na maeneo mengine, kwamba watumiaji wa vyanzo vya maji wengi hivyo lazima  wasimamie na kuwekwa taratibu ili wanaotaka kupata huduma za maji wakiwemo wa shughuli za Kilimo,umeme na matumizi majumbani lazima kuomba vibali ili kila mtumiaji apate kiasi cha maji huku lingine kibaki katika mito kwa matumizi mengine.

Akizungumzaara mara baada ya ziara hiyo,Mwenyekiti wa Jukwaa la wahariri Deodatus Balile alisema, kwa muda mrefu vyombo vya habari vimekuwa vikiandika juu ya ukame,upungufu wa maji, mgao wa maji katika Jiji la Dar es salaam lakini mara kwa mara vimekuwa vikirejea suluhisho la tatizo hilo ni ujenzi wa bwawa la Kidunda.

"Baada ya vyombo vya habari kuandika kwa mfululizo Serikali chini ya Rais Samia imesikia na kuanza ujenzi wa mradi huu ambao ni mkombozi wa muda mrefu kwa jiji la Dar es salaam,"alisema

Balile alisema, wakati Serikali ikiendela kupongezwa ni vyema vyombo vya habari vikaendelea kueleza bila kuchoka kuwa maeneo mbalimbali hakuna maji kutokana na kukauka kwa maji mto Ruvu na Serikali kusikia

"Miradi kama hiii mikubwa ambayo inahitaji fedha na utaalamu tunaamini kwamba itaendelea kujengwa katika maeneo mbalimbali na hapo Serikali itakuwa imetimiza vyema wajibu wake wa kuwahudumia wananchi ambao ni kuhakikisha wanapata huduma za kijamii.

Mradi wa ujenzi wa bwawa la Kidunda linatarajiwa kukamilika kwake mwezi Juni 2026.


Mwisho.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI