Na Gabriel Kilamlya, Matukio DaimaAPP NJOMBE
WAKATI Halmashauri ya mji wa Njombe ikishika nafasi ya kwanza kwa ubora katika Elimu kwa mkoa wa Njombe serikali imetakiwa kuchukua hatua ya kukabiliana na upungufu wa zaidi ya walimu 600 ili kuinua Zaidi kiwango Cha Taaluma.
Taarifa ya Elimu Halmashauri ya mji wa Njombe iliyosomwa na Ofisa Elimu Taaluma Huruma Chaula kwa niaba ya Mkurugenzi Katika Kikao Cha wadau wa Elimu kikilenga kujadili Hali ya elimu imesema licha ya mafanikio makubwa ya kitaaluma lakini Wana upungufu wa Walimu 623 ambao wakiajiriwa wanaweza kufanya makubwa Zaidi.
Mwalimu Prochesius Mguli ni Ofisa Elimu Sekondari Halmashauri ya Mji wa Njombe ambaye anasema michango na mijadala mizuri ya wadau wa elimu itawasaidia kuona namna bora ya kuendelea kupambana.
Kaimu mkurugenzi wa Halmashauri ya mji wa Njombe Dokta Jabil Juma anasema changamoto zilizopo katika sekta ya Elimu zinapaswa kutatuliwa kwa mijadala yenye tija ili wanafunzi waweze kupata Elimu Bora na hii itachagizwa na Walimu wenye weledi wa kazi
Mwenyekiti wa Halmashauri ya mji wa Njombe Mhe.Erasto Mpete amesema Halmashauri itaendelea kuongeza nguvu katika kuwapa motisha walimu ili wawafundishe kwa moyo watoto ambao wameonekana kuwa na welevu katika masomo yakiwemo ya Sayansi.
Baadhi ya walimu mkoani Njombe akiwemo Jimmy Ngumbuke Mkuu wa shule ya Sekondari Mbeyela anasema wakati serikali ikianzisha shule za amali inapaswa kuongeza nguvu katika kuajiri walimu na miundombinu ya Ufundishaji na ujifunzaji kwani Teknolojia haiepukiki kwa sasa.
Kituo hiki kimezungunza na baadhi ya wanafunzi ambao wanaiomba serikali kuwekeza kwa walimu kwani wanafanya vizuri kwa sababu yao huku Wazazi wakisema mlo kamili Kwa watoto Utasaidia kuepukana na udumavu.
Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Njombe Mhe.Juma Sweda,Ofisa Tarafa ya Igominyi Tumain Nganyangwa anasema serikali inaendelea kufanyia kazi Changamoto zinazoikumba Sekta ya Elimu Kwa kadri inavyowezekana.
Mwisho.
0 Comments