NA BERDINA MAJINGE, MATUKIO DAIMA
Mjumbe wa halmashauri kuu ya CCM Taifa{ NEC} ambaye pia Mwenyekiti wa usalama barabarani Mkoa wa Iringa Salim Abri Asas amesema mafunzo ya udereva yana umuhimu kwa waendesha vyombo vya moto barabarani kwa sababu husaidia kupunguza ajali za barabarani.
Salim Asas amesema hayo leo feb 28,2025 wakati wa maadhimisho ya miaka 50 ya ufundi stadi na miaka 30 ya chuo cha ufundi na kubainisha kuwa katika udereva kuna baadhi ya sheria na alama za barabarani hubadilika kutokana na nyakati.
Alisema kuwa asilimia kubwa ya ajali barabarani ni uzembe wa madereva na kutojua sheria za barabarani kwa kukosa uelewa wa alama na sheria za barabarani na kufabya makosa kwa uzembe.
"kila mara hata vyombo vya moto huwa vinabadilika kwa wale waliosoma siku za nyuma ni vyema wakaja tena kujifunza, na wale waliopata leseni bila mafunzo ni muda sahihi wa kwenda veta kujifunza mafunzo ya usalama barabarani ambayo yatasaidia kupunguza ajali barabarani".
Alisema kuwa Iringa ni moja kati ya mikoa ya kwanza kupata chuo cha ufundi kwa miaka 30, chuo hicho kimetoa wanafunzi wengi na wamepata ajira wengine wamejiajiri ikiwa ni moja kati ya ilani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) kuweza kuwasaidia vijana kupata mafunzo kwa vitendo.
"Mafunzo haya ya vitendo yatawasaidia kujiajiri ikiwa ni pamoja na kuongeza ujuzi wanaoupata kutokana na mafunzo yapatikanayo chuoni hapo iliwaweze kujitegemea wenyewe".
kwa upande wake Mwenyekiti cha CCM mkoa wa Iringa Daud Yassin alisema kuwa wajumbe wa halmashauri kuu wamechukua nafasi ya kupata mafunzo japo kwa mda mfupi ilikuwezakujua hasa sheria na alama za usalama barabarani.
"Sisi tumejifunza udereva miaka ya nyuma tulukuwa tunaendesha kwa kutumia uzoefu na kipindi hicho vyombo vya moto vilikuwa vichache bajaji,bodaboda hazikuwepo na sheria nyingi hazikuwepo, maeneo mengi taa za barabarani hazikuwepo"alisema
Alisema kuwa mafunzo hayo yatawasaidia viongozi kupata mwanga na kuzitambua sheria na alama za barabarani mtu akiendesha chombo cha moto kwa tofauti unatakiwa umwambie apunguze mwendo kuepuka ajali za barabarani

Huku akiipongeza serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kutoa fedha nyingi kwa ajili ya miradi ya ujenzi wa vyuo vya ufundi ndani ya mkoa wa Iringa.
.
Mkuu wa chuo cha ufundi veta Iringa Pasience Nyoni amesema chuo cha Veta iringa kilianzishwa mwaka 1987 kikiwa na fani 10 lakini mpaka sasa chuo hicho kinafani 12 na wastani kwa mwaka wanatoa wahitimu 200 mpaka 250
Nyoni alisema kuwa kati ya wahitimu hao 250 ni wale wa mafunzo ya mda mrefu lakini pia chuo kinatoa mafunzo ya muda mfupi.

0 Comments