Header Ads Widget

Wakulima wa Pamba Nyang'hwale wapewa Elimu Kudhibiti Wadudu wa Pamba.


Afisa Kilimo kutoka Bodi ya Pamba Tanzania (TCB), Nicholas Lutema alitoa Elimu ya Kudhibiti Wadudu Kwa wakulima wa Pamba Kijiji Cha Ikangala wilayani Nyang'hwale.


Na Costantine Mathias-Geita.


WAKULIMA wa Pamba katika Kijiji cha Ikangala wilayani Nyang'hwale Mkoa wa Geita wameendelea kupokea Elimu ya Matumizi sahihi ya viuawadudu ili kudhibiti wadudu kama chawa Jani na funza wanaofyonza na kutafuna vitumba vya Pamba.


Afisa Kilimo kutoka Bodi ya Pamba Tanzania (TCB), Nicholas Lutema amesema wanatoa mafunzo hayo kwa wakulima wa Pamba kudhibiti wadudu kwa kuzingatia kalenda ya kilimo zao hilo.


Amesema Elimu ya sahihi ya Viuawadudu na vinyunyizi humsaidia Mkulima kufanya shuguli za upuliziaji kwa ufanisi kudhibiti wadudu wanaoharibu Pamba.


Kutokana na Umuhimu wake, mafunzo haya hutolewa kila msimu wa kilimo na Maafisa Kilimo wa Bodi ya Pamba waliopo katika wilaya 56 na Halmashauri 64 zinazolima zao la Pamba nchini.





Mwisho.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI