Header Ads Widget

UWT, MBUNGE MBARALI WATUMA UJUMBE KWA WAPINZANI 2025.


 

Jumuiya ya wanawake wa Chama Cha Mapinduzi CCM (UWT) Wilaya ya Mbarali, imeadhimisha miaka 48 ya CCM kwa kufanya shughuli mbalimbali ikiwemo kutembelea miradi na kutoa msaada wa vitu mbalimbali hospitalini na shuleni.

Katika maadhimisho hayo, UWT imewataka wanawake na wana CCM kwa ujumla kujiandaa kwa ajili ya uchaguzi mkuu wa mwaka huu.




Akizungumza kwenye maadhimisho hayo katika kata ya Lugelele wilayani humo, mwenyekiti wa jumuiya ya wanawake wa CCM wa Wilaya hiyo Zabibu Nuroo, amesema wanawake wa wilaya yake wanaye mgombea mmoja tu wa ubunge katika jimbo hilo ambaye ni Mbunge wa sasa Mhe. Bahati Keneth Ndingo huku akisema kwa ngazi ya Taifa hakuna mjadala kwani tayari Dkt. Samia Suluhu Hassan alishapitishwa kuwa mgombea wa nafasi ya Rais baadaye Oktoba 2025.

"Muwaambie wasitusumbue (bila kuwataja akina nani), Wanawake tumeweka misimamo mgombea wetu ni mwanamke mwenzetu naye ni Bahati Ndingo (Bahati Ndingo - Mbunge Mbarali), sisi wanawake wa jimbo la Mbarali tunakupenda sana. Ndugu zangu wanawake tunawashukuru sana. Niwaombe tu ndugu zangu wanawake tupendane, tushirikiane, tushikamane, tuzipende familia zetu, akina mama tusibweteke majumbani tutoke twende mashambani tukatafute ridhiki", amesema Bi. Zabibu, Mwenyekiti wa UWT wilaya ya Mbarali huku akiwapongeza wanawake kwa kufanikisha maadhimisho hayo.

Kwa upande wake Mbunge wa jimbo la Mbarali Mhe. Bahati Keneth Ndingo, amewapongeza wanawake kwa kuungana kuadimika miaka 48 ya CCM na kueleza miradi mbalimbali inavyotekelezwa na Serikali hasa miradi ya maji, barabara n huduma ya nishati (umeme) wilayani humo, nishati ambayo sasa imesalia vitongojini pekee.




Amesema wakati watu wengine wakitoa lugha mbaya au matusi wana CCM waendelee kusema kazi zinazofanywa na CCM kwa maslahi ya wananchi na inapofika kipindi cha uchaguzi mkuu wakamchague Dkt. Samia Suluhu Hassan na wagombea wa CCM kuwa viongozi wao kwakuwa wana sera bora na zinazotekelezeka.
Pamoja na yote katika maadhimisho hayo, Mbunge wa Mbarali na umoja wa wanawake hao wilayani humo wametoa msaada wa vitu mbalimbali ikiwemo mitungi ya gesi kwa akina mama ntilie, vifaa vya masomo kwa watoto wa mahitaji maalum katika shule ya msingi Igomelo na kwa hospitali ya wilaya ya Mbarali huku pia wana CCM wakifanya pia usafi katika kituo cha afya Rujewa.

Maadhimisho ya miaka 48 ya CCM kitaifa yanatarajiwa kufanyika Februari 05, 2025 jijini Dodoma na mgeni rasmi anatarajiwa kuwa mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Taifa Ndugu Samia Suluhu Hassan.






Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI