Msanii wa Bongo fleva na Mmiliki wa 7media Clinton Chipando (Baba levo) ametangaza kuzunguka mikoa 15 kwa ajili ya kutangaza miradi mikubwa ya maendeleo iliyofanywa na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassani.
Akizungumza na waandishi habari leo jijini Dar es Salaam, amesema kuwa lengo la ziara hiyo ni kuzunguka na waandishi wa habari za mtandaoni (Online Tv) kutangaza miradi mbalimbali ikiwemo Umeme, Maji, Afya na Miundombinu ya barabara.
Amesema Rais Dkt Samia amefanya miradi mikubwa sana ndani ya miaka minne hivyo ni wakati wa wananchi kuweza kutambua miradi hiyo na kumpongeza kwa juhudi aliyoyatenda katika kipindi cha uongozi wake.
"Tunataka kuwaonesha watanzania kuwa mama amefanya mambo makubwa 'Mama huna deni' hii ni kauli mbinu yetu tutakwenda kuiitangaza miradi mikubwa aliyoyafanya na tutamuunga mkono "
Ameongeza"najua katika safari hii watatokea watu kutusema sisi ni chawa lakini sisi hatujali lengo letu ni kutangaza na kumuunga mkono Rais Dkt Samia wetu mpenda maendeleo"
Aidha, amesema ziara hiyo itatoa fursa kwa wabunge, madiwani kutangaza miradi yao walioyafanya na kuiitangaza kwa wananchi.
Sambamba na hayo amesema zipo kampuni ambazo zitashiriki kuwasapoti katika ziara hiyo ikiwa ni pamoja na Madasi Store, Magic builders internation na Jema Auto.
0 Comments